Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shearer: Arteta anajifukuzisha!

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal iliangukia pua kwa kuchapwa na West Ham United kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu England, mechi ambayo ilihitaji kushinda ili kupunguza pengo la pointi lililopo baina yao na vinara Liverpool.

LIVERPOOL, ENGLAND: GWIJI wa Ligi Kuu England, Alan Shearer anaamini kocha Mikel Arteta anatafuta mwenyewe njia ya kujiweka kwenye presha ya kufutwa kazi kwenye klabu ya Arsenal baada ya kushindwa kuifanya timu hiyo kuendelea kufukuzana na Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Arsenal iliangukia pua kwa kuchapwa na West Ham United kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu England, mechi ambayo ilihitaji kushinda ili kupunguza pengo la pointi lililopo baina yao na vinara Liverpool.

Kuona kupoteza kwa West Ham haikuwa bahati mbaya, Arsenal ilikwenda kubanwa tena kwa kutoka sare na Nottingham Forest, hivyo kuipa Liverpool fursa ya kufungua pengo la pointi kuwa kubwa zaidi na kufikia 13.

Kwa hali ilivyo, Arsenal kuna uwezekano mkubwa ikaishia kumaliza kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England na itakuwa kwa mara ya tatu mfululizo.


Arsenal ilishindwa kusajili straika mpya kupitia dirisha la Januari, licha ya Kocha Arteta kuweka hadharani mpango wa kusajili fowadi mpya baada ya waliokuwapo, Gabriel Jesus na Kai Havertz kuwa majeruhi. Tangu Arsenal ipoteze wachezaji hao pamoja na Bukayo Saka imekuwa na matatizo makubwa katika upatikanaji wa mabao, huku Arteta akijaribu washambuliaji kadhaa akiwamo kiungo Mikel Merino.

“Je, Mikel Arteta amejiweka kwenye presha kwa sasa? Hebu niambieni ni kocha gani wa Ligi Kuu England ambao hana presha,” alisema Shearer.

“Lakini, unachoweza kusema ni namna Arsenal ilivyotumia muda wake katika mbio za kufukuzia ubingwa. Hakuna ubishi kwamba ni kocha mwenye kipaji, lakini sioni kama ana presha yoyote ya kutaka mafanikio. Lakini, kibarua chake kitakuwa katika presha kubwa kutoka sasa hadi mwisho wa msimu na msimu ujao.

“Wachezaji wangapi anahitaji kuwaongeza kikosini, lakini kitu kimoja anachopaswa kuanza nacho ni kusajili mshambuliaji wa kati. Arsenal inahitaji straika.”

Kushindwa kusajili katika dirisha la Januari kunaigharimu Arsenal kwa sasa kwa mujibu wa Shearer kutokana na anachoamini kwamba wiki tatu zilizopita, Arsenal ilikuwa timu iliyobeba matumaini makubwa ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, kwamba ingeipa wakati mgumu Liverpool iliyopo kileleni.