Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sesko, Man United kuna  kitu kinakuja

SESKO Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Kocha Ruben Amorim kinahitaji straika mpya dirisha hili la majira ya kiangazi ili kuja kuongeza nguvu kwenye fowadi yao.

LONDON, ENGLAND: NAFASI ya Manchester United kunasa saini ya straika Benjamin Sesko imezidi kuongezeka baada ya staa huyo mwenyewe kuvutiwa na mpango wa kwenda kukipiga kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Old Trafford.

Kikosi hicho cha Kocha Ruben Amorim kinahitaji straika mpya dirisha hili la majira ya kiangazi ili kuja kuongeza nguvu kwenye fowadi yao.

Orodha ya mastraika kibao wamehusishwa na Man United, ikiwamo Viktor Gyokeres, ambaye msimu ujao atakuwapo kwenye Ligi Kuu England baada ya kujiunga na Arsenal.

Sesko sasa anatazamwa kama chaguo jingine bora hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri huko RB Leipzig misimu ya karibuni.

Newcastle pia inamtaka Sesko ikimtazama kama mbadala sahihi wa Alexander Isak, anayehusishwa na mpango wa kutimkia Liverpool.

Lakini, sasa Man United ipo mstari wa mbele kwenye mchakamchaka wa kupata huduma ya straika Sesko.

Kwa mujibu wa Sky ya Ujerumani, mabosi wa Man United wameshanza kuwasiliana na Sesko kumweleza mpango wao. Na wameshabainisha ofa yao kwa mawakala wa mchezaji huyo ili kuanzisha mazungumzo na Leipzig.

Bahati kwa Man United, Sesko amelipokea hilo vyema baada ya kuvutiwa na kile ambacho ameambiwa. Kazi iliyobaki kwenye dili hilo ni kuhusu ada ya uhamisho, Leipzig inahitaji Pauni 64 milioni kwenye mauzo ya fowadi wao huyo.

Kocha Amorim alishazungumza kuhusu kitu anachokitaka kwenye mpango wake wa kusajili nyota wapya, akisema: “Lazima watake wenyewe kuja.

Nadhani tunachoweza kufanya kwa mashabiki ni kuleta wachezaji ambao tayari wameshafanya kitu fulani. Kwa wachezaji wote wanaokuja, tutataka kuzungumza na mchezaji huyo, kumwelezea mipango. Na kingine muhimu, mchezaji mwenyewe awe tayari kuja.”€

Sesko, ambaye alifunga mabao 39 kwenye kikosi cha Leipzig kwa misimu miwili iliyopita, alishaweka wazi kile kitakachomfanya afanye uamuzi ni staili ya uchezaji, alisema: “Kitu muhimu kwangu kwenda kwenye timu inayocheza soka staili ninayoweza kumudu vyema. Nishafahamu kitu cha kufanya.”

Man United imeshawekeza pakubwa kwenye kuboresha safu ya ushambuliaji kwa kuwanasa Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwa ada ya pamoja ya Pauni 133.5 milioni.