Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sesko abadili upepo ghafla

SESKO Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa RB Leipzig amekuwa katikati ya vita kali baina ya klabu hizo mbili za Ligi Kuu England, zote zikihitaji huduma yake.

MUNICH, UJERUMANI: STRAIKA, Benjamin Sesko amechagua kujiunga na Newcastle United badala ya Manchester United, kwa mujibu wa ripoti kutoka Slovenia.

Staa huyo wa RB Leipzig amekuwa katikati ya vita kali baina ya klabu hizo mbili za Ligi Kuu England, zote zikihitaji huduma yake.

Lakini, Newcastle inaripotiwa kushinda vita hiyo kwa taarifa za kutoka huko kwao straika huyo wa Bundesliga.

Kwa mujibu wa Delo, Sesko ameamua kwenda kujiunga kwenye chama la Eddie Howe lenye maskani yake St James’ Park na hivyo kufanya Newcastle kushinda vita mbele ya Man United katika msako wa straika huyo wa moto Ulaya.

Sesko ameripotiwa kuwa na makubaliano na klabu yake kwamba haitamzuia kuondoka endapo kama ofa nzuri italetwa.

Klabu hizo mbili zote zimezungumza na mawakala wa Sesko na wakati ikifahamika Man United inahitaji saini yake, shida inakuja kwenye pesa. Man United inaripotiwa kwenda kwa mabosi wa Leipzig ikiwataka wapunguze bei ya straika huyo, iliyoripotiwa kuwa ni Pauni 70 milioni na bonasi juu.

Sesko, ambaye alihusishwa pia na Arsenal, amefunga mabao 39 katika mechi 87 alizochezea RB Leipzig tangu alipojiunga na miamba hiyo akitokea RB Salzburg miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, wakati ripoti za Slovenia zikisema kwamba Sesko amechagua kwenda kujiunga na Newcastle, hakuna uamuzi wowote rasmi uliofikiwa. Awali, Man United ilionekana kuwa kwenye nafasi kubwa ya kunasa huduma ya straika huyo, lakini Newcastle inampa fursa ya kucheza michuano ya Ulaya msimu huu.

Man United haijafuzu michuano yoyote ya Ulaya msimu huu, hivyo itahitaji kutumia mbinu kali sana kunasa saini ya straika wa aina ya Sesko.

Mchakato huo wa Man United unasimamiwa na mkurugenzi wa usajili, Christopher Vivell, ambaye aliwahi kufanya kazi na Sesko huko RB Salzburg, ambaye alimwelezea straika huyo mwenye kimo cha futi 6 na inchi 5 na kila ubora wa kuwa mmoja wa mastraika matata duniani kwa miaka ya baadaye.

Sesko alifunga mabao 21 kwenye michuano yote aliyocheza msimu uliopita na ana mabao 16 aliyofunga katika mechi 41 alizocheza Slovenia.