Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serbia yatishia kujitoa Euro 2024

Muktasari:

  • Taarifa ya katibu mkuu wa shirikisho la soka la nchi hiyo, Jovan Surbatovic ilisema kujitoa kwa nchi hiyo kunatokana na namna mashabiki wa mataifa hayo mawili wanavyoshangilia.

HUMBURG, UJERUMANI: SERBIA imetishia kujiondoa katika michuano ya Euro 2024, ikizishutumu Croatia na Albania kuwa na kampeni za kutaka kuwafanyia mambo mabaya.

Taarifa ya katibu mkuu wa shirikisho la soka la nchi hiyo, Jovan Surbatovic ilisema kujitoa kwa nchi hiyo kunatokana na namna mashabiki wa mataifa hayo mawili wanavyoshangilia.

Ilieleza mashabiki wa Albania na Serbia walikuwa wakiimba 'ua ua ua Waserbia' katika mchezo uliozikutanisha mataifa hayo mawili na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Surbatovic alisema hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kuwasilisha malalamiko Uefa wakitaka Croatia na Albania wapewe adhabu kwa kauli hizo za mashabiki wao na ikiwa ombi lao halitasikilizwa watakuwa tayari kujiondoa katika michuano hii inayoendelea huko Ujerumani.

"Kwanza kabisa tungependa kuwashukuru mashabiki wetu kwa sapoti yao waliyotuonyesha kwenye mechi dhidi ya England, nina imani watafanya hivyo pia dhidi ya Slovenia."

"Kilichotokea hakikubaliki na tunaiomba Uefa ichukue hatua, ikiwezekana hata iwaondoe katika mashindano, tuna uhakika wataadhibiwa kwa walichokifanya kwa sababu wameshasikiliza ombi letu la kwanza la kumwondoa mwandishi mmoja kutoka Albania kuripoti michuano."

"Tunataka Uefa iadhibu mashirikisho yote ya nchi hizi, hatutaki kwenda mbali zaidi lakini kama hawatoadhibiwa, tutachukua hatua nyingine."

"Mashabiki wetu wamekuwa wakionyesha tabia nzuri sana, ingawa mmoja wao ameadhibiwa kwa vitendo vya ubaguzi, lakini hiyo haiondoi ukubwa wa tabia nzuri tuliyoinyesha na nawasihi mashabiki wetu kuwa watulivu."

Serbia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya England kwa kuchapwa bao 1-0, kundi C na kwa mujibu wa sheria za Uefa ikiwa Serbia itajiondoa kabla ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Denmark, Uefa itawazawadia Danes ushindi wa mabao matatu na pointi tatu kisha Serbia itapigwa faini na inaweza kufungiwa.