Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Senegal yapiga tatu, Jackson atupia mbili

SENEGAL Pict

Muktasari:

  • Mabao mawili ya Nicolas Jackson aliyefunga katika kila kipindi na moja la mtokea benchini Cherif Ndiaye yalitosha kukifanya kikosi cha Simba wa Teranga kukusanya pointi zote tatu katika mechi hiyo na hivyo kushikilia usukani wa kundi.

TANGIER, MOROCCO: MABINGWA wa Afcon 2021, Senegal wameanza kwa kishindo msako wa kusaka ubingwa wa Afcon 2025 baada ya kuitandika Botswana mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi D uliofanyika uwanjani Stade Ibn-Batouta, Jumanne.

Mabao mawili ya Nicolas Jackson aliyefunga katika kila kipindi na moja la mtokea benchini Cherif Ndiaye yalitosha kukifanya kikosi cha Simba wa Teranga kukusanya pointi zote tatu katika mechi hiyo na hivyo kushikilia usukani wa kundi.

Matokeo hayo yanaakisi hisia za wengi kwamba Senegal ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa mashindano hayo ya Morocco kutokana na kuwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wengi wenye viwango bora.

Botswana ilionekana kuzidiwa kwenye idara nyingi katika mechi hiyo ikiwa haijapiga shuti lolote kulenga golini, huku Senegal ikipoteza nafasi nyingi za kufunga kupitia kwa Jackson na mshambuliaji wao nguli, Sadio Mane.

Senegal ilipiga mashuti 23 katika mechi hiyo, huku 17 yakilega goli, wakati kwa upande wa Botswana kwa mechi yote, ilipiga mashuti matatu tu na hakuna hata moja lililolenga golini.

SENE 01

Mechi hiyo ilionekana kama vile ya upande mmoja, ambapo Senegal ilimiliki mpira kwa asilimia 67 dhidi ya 33 za Botswana, ambayo kipa wake, Goitseone Phoko alifanya sevu 14, wakati Edouard Mendy alikuwa na wakati mzuri uwanjani, kwa sababu hakufanya sevu yoyote kutokana na muda mwingi hakuwa kwenye purukushani za kukabiliana na mashambulizi ya wapinzani kutokana na ukuta imara wa beki yake iliyokuwa ikiongozwa na mwili jumba, Kalidou Koulibaly.

Mchezo wa mapema kwenye kundi hilo, DR Congo iliichapa Benin 1-0, shukrani kwa bao la Theo Bongonda.


MECHI ZIJAZO ZA KUNDI D

Desemba 27, 2025

Benin   v Botswana     (Saa 9:30 alasiri)

Senegal           v DR Congo      (Saa 12:00 jioni)


Desemba 30, 2025

Benin   v Senegal                    (Saa 4:00 usiku)

Botswana        v DR Congo      (Saa 4:00 usiku)