Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Koulibaly: Siwezi kulinganisha AFCON na Kombe la Dunia 

KOULLIBALY Pict

Muktasari:

  • Senegal ni miongoni mwa mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la AFCON 2025 na pia inatazamwa kwa macho mawili kwenye mbio za kusaka ubingwa wa Kombe la Dunia 2026, huku kauli ya Koulibaly ikionyesha wazi vipaumbele, malengo na shauku ya kizazi cha sasa cha wachezaji wa Simba wa Teranga.

Beki na nahodha wa Senegal, Kalidou Koulibaly, amesema hawezi kufananisha hatua ya kufuzu Kombe la Dunia na kutwaa ubingwa wa AFCON, akisisitiza kuwa mashindano ya dunia yana uzito wa kipekee kwa wachezaji, taifa na kizazi kizima cha wapenda soka.

Akizungumza nchini Morocco, Koulibaly amesema AFCON ni mashindano makubwa na ya heshima barani Afrika, lakini Kombe la Dunia linabeba ndoto pana zaidi na hadhi ya kimataifa ambayo haiwezi kulinganishwa na mashindano mengine yoyote.

“AFCON ni mashindano muhimu sana, ni fahari kubwa kwa taifa la Afrika kubeba ubingwa wa AFCON. Lakini Kombe la Dunia ni mashindano yenye hadhi kubwa, na ni ndoto ya kila mchezaji kucheza mashindano hayo tangu akiwa mdogo. Sitaweza kulinganisha hatua ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kutwaa taji la AFCON,” amesema Koulibaly.

Beki huyo wa kati wa kikosi cha Senegal, ameongeza kuwa kufuzu Kombe la Dunia hutoa fursa kubwa kwa wachezaji kuonekana kimataifa, kukuza thamani ya soka la taifa husika na kuhamasisha kizazi kipya kwa wachezaji.

KOUL 01

Koulibaly, ambaye aliiongoza Senegal kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa AFCON mwaka 2021, amesema mafanikio hayo yalikuwa ya kihistoria, lakini safari ya Kombe la Dunia hubeba presha, heshima na motisha.

“Kombe la Dunia linaiweka nchi yako kwenye ramani ya dunia. Ni mashindano ambayo yanatazamwa na kila mtu, na hatua ya kushiriki tu, tayari ni ushindi mkubwa. Ndiyo maana wachezaji wengi wako tayari kupigania kufuzu hata kuliko mataji mengine,” ameongeza.

Hata hivyo, Koulibaly amesisitiza kuwa, kauli yake haimaanishi kudharau AFCON, akieleza kuwa Senegal itaendelea kupambana kwa nguvu zote katika mashindano yote mawili.

KOUL 02

“Hatuchagui mashindano. Tunataka kushinda kila tunachoshiriki. AFCON ni fahari ya Afrika, Kombe la Dunia ni ndoto ya dunia. Kama timu kubwa, lazima tupiganie vyote,” amesema.

Senegal ni miongoni mwa mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la AFCON 2025 na pia inatazamwa kwa macho mawili kwenye mbio za kusaka ubingwa wa Kombe la Dunia 2026, huku kauli ya Koulibaly ikionyesha wazi vipaumbele, malengo na shauku ya kizazi cha sasa cha wachezaji wa Simba wa Teranga.