Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Santi Cazorla aibua shangwe akitimiza ndoto

CARZOLA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo alisaidia Oviedo kushinda dhidi ya Mirandes na kufanikisha kurejea kwao Ligi Kuu baada ya kukosekana kwa miaka 24, jambo lililosababisha mashabiki kuvamia uwanja kwa shangwe.

OVIEDO, HISPANIA: KIUNGO Santi Cazorla amekamilisha hadithi yake ya ndoto akiwa na Oviedo baada ya kufunga na kuwasaidia kupanda tena LaLiga.

Nyota huyo alisaidia Oviedo kushinda dhidi ya Mirandes na kufanikisha kurejea kwao Ligi Kuu baada ya kukosekana kwa miaka 24, jambo lililosababisha mashabiki kuvamia uwanja kwa shangwe.

Cazorla  alianza maisha yake ya soka katika akademi ya Oviedo mwaka 1996 kabla ya kung’ara akiwa na timu za Villarreal, Malaga na Arsenal.

Staa huyu ambaye alikuwa karibu kushindwa kurejea uwanjani kutokana na majeraha ya kisigino ya mara kwa mara, alirejea Oviedo mwaka 2023 akitokea Qatar.

Wakati huo, Oviedo ilikuwa ikicheza Ligi Daraja la Kwanza Hispania, ikiwa inapambana kurejea tena La Liga baada ya kukosekana tangu mwaka 2001.

Msimu wake wa kwanza baada ya kurejea uliisha vibaya  baada ya kupoteza  fainali ya mchujo wa kupanda daraja.

Lakini sasa timu hiyo ndogo imepanda tena ligi kuu baada ya Cazorla kuiongoza kwa ushindi wa kushangaza dhidi ya wapinzani wao Mirandes, waliokuwa wameanza kwa kuongoza  1-0, lakini Cazorla alisawazisha kwa kufunga penalti kabla ya mapumziko.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza Oviedo ilipokea kichapo cha bao 1-0, hivyo licha ya kusawazisha bado matokeo ya jumla yalikuwa ni 2-1.

Hata hivyo, Oviedo ilipata bao la pili kipindi cha pili na baadae kuongeza msumari wa tatu katika muda wa ziada. Mashabiki waliingia uwanjani kushangilia ushindi huo.

Kiungo huyo alitamani hata asilipwe, lakini kanuni za ligi zilimlazimu akubali mshahara wa chini wa Pauni 80,000 kwa mwaka.

Sasa inasubiriwa kuonekana kama Cazorla atabaki kwa msimu mmoja zaidi kwenye LaLiga, licha ya kupitia upasuaji mara 10 unaomwacha na maumivu ya kila siku.

Staa huyu alikuwa na miaka miwili ya mateso ya majeraha kuanzia mwaka 2016 kiasi cha kupata maambukizi ya bakteria yaliyokula sehemu ya sentimita 10 ya mfupa wa kisigino na kifundo cha mguu wake wa kulia lakini akatibiwa na kupona.

Cazorla alifunga mabao 29 katika mechi 180 katika miaka yake sita Emirates, pia akinyakua mataji mawili ya FA Cup.

Akiwa na timu ya taifa ya Hispania alicheza mechi 81 na kushinda Euro mara mbili mfululizo, lakini alikosa ushindi wa Kombe la Dunia 2010 kutokana na maumivu ya hernia.