Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sancho afunguka kusepa Chelsea, Wasaudia watajwa

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa England alionyesha kiwango bora akiwa na Chelsea baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha Man United.

LONDON, ENGLAND: SUPASTAA wa England, Jadon Sancho amezungumzia kuhusu kuondoka kwake Chelsea baada ya timu hiyo kuilipa Manchester United Pauni 5 milioni ili kutomsainisha mkataba wa kudumu, huku taarifa zikieleza kuwa anaweza kutumkiaAl-Hilal, Al-Ittihad au Al-Nassr ambazo za Saudia Arabia.

Nyota huyo wa zamani wa England alionyesha kiwango bora akiwa na Chelsea baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha Man United.

Sancho aliingia katika mgogoro na kocha wa zamani wa Mashetani wa Wekundu, Erik Ten Hag ambaye alimshutumu kwa kutojituma  mazoezini baada ya kutomjumuisha katika kikosi kilichocheza na Arsenal 2023, jambo ambalo mchezaji huyo alilitaja kuwa “siyo kweli” kwenye chapisho aliloweka katika mitandao ya kijamii na baadaye kulifuta.

Hali hiyo ilisababisha Ten Hag kumtaka Sancho aombe radhi, lakini mchezaji hakukubali na baada ya hapo hakuwahi tena kucheza chini ya kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi, na baadaye akaenda Borussia Dortmund kisha Chelsea.

Lakini, Chelsea ilikuwa na nafasi ya kumsajili kwa mkataba wa kudumu kwa Pauni 25 milioni  kipindi hiki cha majira ya kiangazi, ila badala yake ilichagua kulipa Pauni 5 milioni ili kufuta mkataba huo na Sancho sasa anarudi Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amezungumzia kuhusu kuvunjika kwa mpango wa kuhamia Chelsea huku hatima yake ikiwa bado haijajulikana.

“Upendo mkubwa kwa kila mtu ndani ya Chelsea ulinifanya nijisikie kama nyumbani, wachezaji wenzangu, wafanyakazi na mashabiki. Nawatakia klabu kila la heri mbele. Nashukuru sana, asanteni Blues.”

Ujumbe huo uliambatana na mkusanyiko wa baadhi ya picha za nyakati bora za Sancho akiwa Chelsea zikijumuisha michuano ya Ligi Kuu England na Conference League. Mail Sport iliwahi kufichua kuwa mkataba wa mkopo wa Sancho ulikuwa na kipengele kinachoiwezesha Chelsea kujiondoa kwenye wajibu wa kumnunua kwa kulipa ada ya mamilioni.

Staa huyo alipachika bao katika fainali ya Conference League dhidi ya Real Betis ambayo Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Katika msimu uliopita, Sancho alifunga mabao matano na kutoa asisti 10 kwenye mechi 42 za michuano yote.Mkataba wa Sancho na United unaisha mwaka 2026 na unajumuisha chaguo la kuongezewa mwaka mmoja zaidi.