Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah awindwa tena Saudia Waarabu Saudia

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2023,  Al-Ittihad iliweka mezani ofa ya Pauni 150 milioni kama ada ya uhamisho kumsajili Salah lakini ilikataliwa na Liverpool.

AL-Ittihad Club ya Saudi Arabia ambayo ilishindwa kufanikisha mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah 2023, imerudi mezani ambapo inaitaka huduma ya staa huyo atakayepatikana kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu.

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2023,  Al-Ittihad iliweka mezani ofa ya Pauni 150 milioni kama ada ya uhamisho kumsajili Salah lakini ilikataliwa na Liverpool.

Waarabu hao wamechukua hatua ya kuanzisha tena juhudi zao za kumvutia nyota huyo wa miaka 33, ambaye atakuwa huru kuhamia klabu yoyote baada ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa ripoti, Salah anaondoka Liverpool kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine na hiyo imesababisha kuibuka kwa vigogo wanaoonyesha nia ya kuhitaji huduma yake.

Inaaminika kwamba itakuwa ngumu kwa staa huyu kujiunga na timu yoyote ya Ligi Kuu England kutokana na heshima kubwa aliyojijengea akiwa na Liverpool. Tangu kuanza kwa msimu huu, Salah alicheza mechi 34, amefunga mabao 10 na kutoa asisti tisa.

Mkataba wa sasa wa Salah unatarajiwa kumalizika fikapo 2027, lakini anatarajia kuondoka akiwa mchezaji huru kutokana na makubaliano kati yake na vigogo wa Liverpool.


Casemiro

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Casemiro, 34, anayeichezea Manchester United huenda akatua Marekani ambako timu mbili zimemtafuta kutaka kujua kama zinaweza kumsajili.

Casemiro alitangaza kuondoka Man United mwisho wa msimu jambo lililowahuzunisha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakiimba majukwaani kuwa asiondoke apewe mkataba mpya. Watu wa karibu na Casemiro wanadai anatamani kwenda Marekani.


Michael Olise

LIVERPOOL inadaiwa kuwasiliana na Bayern Munich kuulizia uwezekano wa kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili awe mbadala wa Mohamed Salah.

Hata hivyo, Bayern inaonekana kutokuwa na presha kuhusu mustakabali wa Olise, kwani mchezaji huyo bado ana mkataba hadi 2029 na hana kipengele kinachoilazimisha timu hiyo kumuuza. Hali hiyo inaifanya Liverpool kukutana na kizingiti.


Alessandro Bastoni

BARCELONA imeonyesha nia ya kumsajili beki wa kimataifa wa Italia, Alessandro Bastoni, 26, kutoka Inter Milan.

Hata hivyo, Barca inaweza kukutana na ushindani mkali kutoka Liverpool, ambayo imekuwa ikihitaji kumsajili beki huyo tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Bastoni ni miongoni mwa mabeki bora wa  Serie A kwa sasa na inaelezwa Inter Milan inaweza kuhitaji Pauni 60 milioni ili kumuuza staa huyo.


Marcus Rashford

MANCHESTER United ina imani kuwa itaweza kumpatia timu nyingine mshambuliaji wake, Marcus Rashford, 28, ikiwa Barcelona haitafanya uhamisho wake wa mkopo kuwa wa kudumu.

Barca ina chaguo la kumsajili Rashford kwa Pauni 26 milioni, lakini imekuwa ikisita kutokana na hali ya kiuchumi na imekuwa ikiomba kupunguziwa bei jambo ambalo Man United imelikataa. Hadi sasa mustakabali wa Rashford bado haujajulikana.


Vinícius Jr

WINGA wa kimataifa wa Brazil, Vinícius Júnior, 25, bado anataka kuendelea kubaki Real Madrid kwa muda mrefu.

Inaelezwa Vinicius lengo lake ni kuendelea kuitumikia Madrid na hivi karibuni anatarajiwa kusaini mkataba  mpya wa kuendelea kubaki kikosini hapo.

Awali, Vinicius aliripotiwa anaweza kuondoka mwisho wa msimu ambapo vigogo wa Saudi Arabia wamekuwa wakihusishwa naye.


Moises Caicedo

KIUNGO wa Chelsea, Moises Caicedo  mwenye umri wa miaka, 24, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka Stamford Bridge licha ya kuhusishwa na Real Madrid.

Caicedo, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ecuador anadaiwa kusisitiza kuwa anafurahia maisha yake ndani ya Chelsea na anataka kuendelea kuitumikia klabu hiyo muda mrefu. Kauli hiyo ni pigo kwa klabu zinazomtaka.


Dusan Vlahovic

JUVENTUS ipo karibu kufanikisha dili la kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Serbia, Dusan Vlahovic, 26.

Inaelezwa kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yako katika hatua za mwisho, huku Juventus ikitaka kumbakisha nyota huyo kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Vlahovic ameendelea kuwa tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Juventus.