Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Davies atajwa kutua Manchester United

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Real Madrid ilikuwa karibu kukamilisha dili la kumsajili nyota huyo mwaka jana ambapo mkataba wake ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu, lakini Bayern Munich ilifanikiwa kumshawishi kuongeza mkataba na kubaki katika viunga vya Allianz Arena.

MANCHESTER United imeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Canada, Alphonso Davies, 25, kutoka Bayern Munich katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi.

Inaelezwa kwamba Bayern Munich iko tayari  kupokea ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo, jambo linalofungua mlango kwa Manchester United kujaribu kumsajili.

Hata hivyo, bado haionekani kuwa rahisi kwa Mashetani Wekundu hao kufanikiwa katika dhamira hiyo, kwani Real Madrid pia imekuwa ikitajwa kutaka kuipata huduma ya Davies kwa muda mrefu.

Real Madrid ilikuwa karibu kukamilisha dili la kumsajili nyota huyo mwaka jana ambapo mkataba wake ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu, lakini Bayern Munich ilifanikiwa kumshawishi kuongeza mkataba na kubaki katika viunga vya Allianz Arena.

Mkataba wa sasa wa Davies unatarajiwa kumalizika ifikapi 2030, lakini changamoto anayokutana nayo hivi sasa imekuwa ni majeraha ya mara kwa mara yanayosababisha awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Davies amecheza mechi 13 za michuano yote na kutoa asisti mbili katika mashindano mbalimbali.

Dili lolote litakalofanyika la kutaka kumng’oa mchezaji huyo katika kikosi cha Bayern Munich linaweza kugharimu zaidi ya Pauni 70 milioni au zaidi, hivyo timu zinapaswa kujipanga.


Josh Acheampong

BBEKI wa kulia wa Chelsea, Josh Acheampong, 19, anaonekana kuwa katika rada za Crystal Palace inayotaka kumsajili katika dirisha lijalo.Inaelezwa kuwa Palace inamuona mchezaji huyo kama sehemu ya maboresho ya  kikosi ambacho kimeondokewa na wachezaji wengi tegemeo tangu mwaka jana. Acheampong anadaiwa kuomba kuondoka Stamford Bridge ifikapo mwisho wa msimu huu kutokana na changamoto ya kukosa nafasi ya kucheza.


Jadon Sancho

WINGA wa kimataifa wa England, Jadon Sancho, 25, anayecheza kwa mkopo Aston Villa akitokea Manchester United, amefanya mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu uwezekano wa kurejea katika viunga hivyo vya Signal Iduna Park. Inaelezwa kuwa Sancho yupo tayari hata kupunguza mshahara ili kukamilisha uhamisho huo mwisho wa msimu huu ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika. Inaelezwa Sancho anaamini anaweza akarudi upya.


Ao Tanaka

KIUNGO wa kimataifa wa Japan, Ao Tanaka, 27, anayekipiga katika kikosi cha Leeds United, anawindwa na Schalke 04 na Hannover 96. Inaelezwa Schalke 04 na Hannover 96 zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Tanaka anatamani kuondoka mwisho wa msimu ikiwa Leeds itashindwa kubaki Ligi Kuu England kwani anahitaji kucheza Ligi Kuu msimu ujao.


Bruno Guimaraes

MANCHESTER United imeendelea kuonyesha nia ya kumtaka nahodha wa Newcastle United, Bruno Guimaraes, 28, licha ya kuambiwa ni ngumu kufanikisha hilo. Taarifa kutoka Brazil zinaeleza kiungo huyo anaweza kuuzwa kwa takriban Pauni 60 milioni. Newcastle imeweka wazi kuwa bado inahitaji kuendelea kuipata huduma ya Guimaraes, lakini haitasimama njiani ikiwa mchezaji mwenyewe ataomba kuondoka.


Wilson Isidor

SUNDERLAND bado inatafuta straika mpya itakayemsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuziba pengo linalotarajiwa kuachwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Wilson Isidor, 25, ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka mwisho wa msimu. Isidor anaripotiwa kutaka changamoto mpya baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Uongozi wa Sunderland tayari unaandaa orodha ya mrithi wake.


Ben White

MABOSI wa Arsenal wapo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya beki Ben White katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa itafanikiwa kumsajili beki wa Sporting CP, Ivan Fresneda katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Taarifa zinaeleza benchi la ufundi la Arsenal linaona ujio wa Fresneda utapunguza nafasi ya kucheza kwa White ikizingatiwa ushindani uliopo katika safu ya ulinzi kwa sasa.


Antoine Griezmann

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Antoine Griezmann, 35, anatarajiwa kuhitimisha safari ya miaka 10 ndani ya Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu. Inaelezwa Griezmann yupo mbioni kujiunga na Orlando City ya Ligi Kuu Marekani na tayari ameshafanya makubaliano binafsi. Griezmann amekuwa muwazi muda mrefu kwamba atakapotaka kustaafu soka atahitimishia Marekani.