Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya Guimaraes na Joelinton yageuka shubiri, ndege yageuza angani

GUIMARAES Pict

Muktasari:

  • Wawili hao walitarajiwa kutua mjini Seoul mapema jana Oktoba 7, 2025 kwa ajili ya mazoezi na kikosi cha Brazil, lakini ndege waliyokuwa wakisafiria iligeuka katikati ya safari kutokana na dirisha kupasuka. Rubani alilazimika kurudi Amsterdam kwa sababu za kiusalama.

NYOTA wa Newcastle United, Bruno Guimaraes na Joelinton wamekumbwa na kadhia ya safari wakielekea Korea Kusini kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Brazil inayonolewa na kocha Carlo Ancelotti.

Wawili hao walitarajiwa kutua mjini Seoul mapema jana Oktoba 7, 2025 kwa ajili ya mazoezi na kikosi cha Brazil, lakini ndege waliyokuwa wakisafiria iligeuka katikati ya safari kutokana na dirisha kupasuka. Rubani alilazimika kurudi Amsterdam kwa sababu za kiusalama.

Bruno na Joelinton walikuwa wameshaanza safari kwa takribani saa 12 bila kufika Soul walipokuwa wamekusudia kwenda kujiunga na wachezaji wenzao wa Brazil.

Kutokana na changamoto hiyo, Guimaraes atasafiri kwa ndege nyingine kupitia nchi tofauti na Uholanzi na anatarajiwa kuwa wa kwanza kutua Korea Kusini, huku Joelinton akitarajiwa kusafiri moja kwa moja kutokea Amsterdam.

Brazil wamepanga kufanya mazoezi saa 10 jioni kwa saa za huko kwenye Uwanja wa Goyang, lakini Joelinton hataweza kufika kwa wakati huku ikiwa haijathibitishwa kama Guimaraes naye atawahi mazoezi hayo.

Oktoba 10, 2025, Brazil itachuana na Korea Kusini katika mechi ya kimataifa ya kirafiki, kisha itasafiri umbali wa maili 780 hadi Tokyo kwa ajili ya mechi nyingine dhidi ya Japan itakayopigwa Jumanne ya wiki ijayo.

GUIMA 02

Baada ya michezo hiyo ya kimataifa, Guimaraes na Joelinton watakabiliwa na safari ndefu ya maili 5,768 kurudi Newcastle, England ambapo watasafiri kwa saa 48 tayari kwa mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Brighton itakayochezwa Oktoba 18, 2025.

Kabla ya mapumziko ya kimataifa, Guimaraes alisema: "Mapumziko haya hayajaja katika wakati mzuri sana kwetu, kwa sababu tulikuwa kwenye kasi nzuri.

"Lakini sasa tunalazimika kwenda kwenye majukumu ya kimataifa, kucheza vizuri na kurudi tukiwa fiti kwa ajili ya mchezo muhimu unaokuja.

"Ninaenda Korea Kusini ni jambo la ajabu, lakini ni lazima. Kuitumikia nchi yangu, ni fahari kubwa kwangu, lakini ni mbali sana."

GUIMA 01

Newcastle United ilishinda 2-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mechi yao ya mwisho kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Lakini nyota wenzao wa Brazil, Igor Jesus na John Victor waliokuwa kwenye kikosi cha Notingham Forest tayari wamewasili Seoul na wameshiriki mazoezi ya jana Jumanne Oktoba 7, 2025.