Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi mpya Arsenal kumvuta Guimaraes

BOSI Pict

Muktasari:

  • Arsenal imeweka bayana Berta, bosi wa zamani wa Atletico Madrid, kuwa chaguo lao kwenye kurithi mikoba ya Edu katika nafasi ya mkurugenzi wa michezo baada ya Mbrazili huyo kung'atuka.

LONDON, ENGLAND: BOSI mpya atakayesimamia usajili Arsenal, Andrea Berta yupo tayari kumvuta kikosini Bruno Guimaraes ikiwa ni sehemu ya kuunda upya safu ya kiungo ya timu hiyo na kuleta watu wa maana.

Arsenal imeweka bayana Berta, bosi wa zamani wa Atletico Madrid, kuwa chaguo lao kwenye kurithi mikoba ya Edu katika nafasi ya mkurugenzi wa michezo baada ya Mbrazili huyo kung'atuka.

Berta atakuwa na kazi ya kutambua na kusajili wachezaji wenye uwezo kuibadili Arsenal na kuifanya timu hiyo kuwa ya kushindania mataji. Wakati ikifahamika kwamba klabu itaweka nguvu kwenye usajili wa straika, kinachoonekana kuna mpango mwingine pia kwenye ishu hiyo ya usajili.

Ilielezwa Januari mwaka huu kwamba kiungo Martin Zubimendi amewekwa kwenye mpango wa kutua Arsenal mwishoni mwa msimu huu - lakini bado Arsenal itaingia kwenye vita ya kumnasa Guimaraes.

Ripoti zinafichua, Berta amekuwa akivutiwa kwa muda mrefu na kiungo Guimaraes na aliwahi kufanya jaribio la kumsajili kiungo huyo wa Newcastle United mara tatu huko nyuma.

Kutokana na Jorginho na Thomas Partey wote mikataba yao kumalizika mwisho wa msimu na wakijiandaa kuondoka, Berta anaweza kurudi tena kwenye msako wa huduma ya Guimaraes.

Guimaraes amekuwa na furaha kubwa huko Newcastle, ambako amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu aliyokuwa huko.

Kinachoelezwa ni kwamba Guimaraes na Newcastle zimekuwa na makubaliano kwamba anaweza kuondoka kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni 60 milioni endapo kama klabu hiyo itashindwa kufuzu mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kama Arsenal itawasajili Guimaraes na Zubimendi kwenye dirisha lijalo, hilo litamfanya kocha Mikel Arteta kuwa na machaguo ya kutosha kwenye safu yake ya kiungo kutokana na kuwa na huduma ya wakali wengine matata, Martin Odegaard, Declan Rice na Mikel Merino.

Myles Lewis-Skelley naye pia anatarajia kutumika kwenye eneo kushoto. Arsenal inavutiwa na mchezaji mwenzake Guimaraes, straika Alexander Isak, wakihitaji huduma ya Namba 9 huyo aende kuboresha fowadi yao.