Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sadio Mane atoa stori ya Jurgen Klopp

HALAAND Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Senegal alikuwa na wakati mzuri chini ya Klopp kwenye kikosi cha Liverpool kwa kipindi cha miaka minane baada ya kumsajili kwa ada ya Pauni 34 milioni akitokea Southampton 2016.

MUNICH, UJERUMANI: STAA Sadio Mane amefichua kwamba ameombwa radhi na kocha Jurgen Klopp baada ya kushindwa kumsajili wakati akiwa Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Fowadi huyo wa Senegal alikuwa na wakati mzuri chini ya Klopp kwenye kikosi cha Liverpool kwa kipindi cha miaka minane baada ya kumsajili kwa ada ya Pauni 34 milioni akitokea Southampton 2016.

Hata hivyo, Mane na Klopp ilionekana wangeweza kuwa pamoja miaka kadhaa nyuma huko Bundesliga. Klopp alikuwa akiinoa Dortmund 2014 wakati alipotambua uwezo wa Mane, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akikipiga Red Bull Salzburg.

Klopp alijaribu kumsajili Mane akakipige Dortmund, lakini dili hilo lilikwama na matokeo yake, Msenegali alitimkia zake Southampton kabla ya Klopp kutua Liverpool kwenda kuchukua mikoba ya Brendan Rodgers.

Mane amesema: “Nilikutana na Klopp. Alitaka kunisajili niende Dortmund, lakini hilo lilikwama.”

Wawili hao walipishana njia kwa miaka miwili kabla ya kukutana kwenye Ligi Kuu England, ambapo Klopp aliona ulikuwa wakati mwafaka wa kufanya kazi pamoja kwenye ardhi ya England kuliko Ujerumani, wakati Mane aliposema: “Klopp alipokuja Liverpool na mimi nilikuwa Southampton. Tukakutana tena. Alinipigia simu na kuniambia, sikia ilishindikana kule lilikuwa kosa langu, je unafikiriaje kwa sasa? Tunaweza kufanya kazi pamoja. Kisha nilienda kukutana na Mauricio Pochettino huko Tottenham. Nilimjibu sawa, kwanza kubaliana na wakala wangu kila kitu. Nitakuja Tottenham. Niliporudi nyumbani, siku tatu baadaye, Klopp alinipigia, nilimuuliza huyu ni Klopp? Hii ni sahihi, nataka huu uhamisho. Nilimhakikishia kuna timu zinanitaka, lakini nakuja hapo.”

Baada ya kujiunga na Liverpool 2016, Mane alifunga mabao 120 na kuasisti 46.