Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mane afichua kwa nini aliikataa Man United na kutimkia Anfield

MANE Pict

Muktasari:

  • Mane amefichua jambo hilo, ambalo huenda mashabiki wengi wa soka walikuwa hawalifahamu kutokana na tabia yake ya ukimya, lakini ameamua kufanya hivyo ili kuiweka wazi sehemu ya historia ya soka lake hasa alipokuwa anacheza katika Ligi ya EPL.

Hatimaye mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Sadio Mané, amefichua kuwa alikataa kusajiliwa na Manchester United na badala yake akaamua kujiunga na Liverpool mwaka 2016.

Mane amefichua jambo hilo, ambalo huenda mashabiki wengi wa soka walikuwa hawalifahamu kutokana na tabia yake ya ukimya, lakini ameamua kufanya hivyo ili kuiweka wazi sehemu ya historia ya soka lake hasa alipokuwa anacheza katika Ligi ya EPL.

Kwa wakati huo, Mané alikuwa akizivutia timu nyingi, kufuatia kiwango bora alichokionyesha akiwa na Southampton, na hatimaye akaamua kujiunga na kwa Liverpool iliyomsajili kwa Pauni 30 milioni.

MAN 01

Mshambuliaji huyo kutoka Senegal, amesema alichukua uamuzi huo, kutokana na ahadi za aliyekuwa kocha wa Man United kwa wakati huo Louis van Gaal, ambazo anadai hazikumvutia.

Amesema kutokana na hatua hiyo, alichukuwa uamuzi wa kusajiliwa na Liverpool ambayo ilimwekea wazi mpango mkakati mezani na hatimaye alifanikiwa kuwa sehemu ya kikosi kilichoipa taji klabu hiyo ya Liverpool msimu wa 2019/2020.
 
“Manchester United walinipigia simu wakati huo, nilikuwa nikizungumza na van Gaal. Wayne Rooney alikuwa pale. Na Angel Di María alikuwa pale. Na Memphis Depay pia,” Mané amesema kwenye Rio Ferdinand Presents.
 

MAN 02


“Sikupendezwa na mipango yao kwa sababu sikuona kana inaonyesha kitu ambacho kingenipa mafanikio katika soka la England, niliamua kujiunga na Liverpool kwa sababu uongozi wake ulinishawishi kwa mambo mengi ikiwepo mipango ya mafanikio, na nilifanikiwa nikiwa na wachezaji wenzangu pala Anfield.”

“Nakumbuka baada ya kuikataa Man United, walijipanga kwa mchezaji mwingine ambaye ni Anthony Martial na walifanikiwa kumsajili kama mbadala wa mpango ambao ulishinda kunishawishi,” amesema

Akiwa Liverpool Mané alicheza mechi 269 kufunga mabao 120 kabla ya kuondoka Anfield na kuelekea Bayern Munich mwaka 2022.