Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rooney awaweka Semenyo, Mbeumo, Gyokeres pamoja

Muktasari:

  • Gyokeres, 27, alijiunga na Arsenal kwenye dirisha lililopita akitokea Sporting Lisbon amefunga mabao sita katika mechi 14.

LONDON, ENGLAND: WAYNE Rooney amemtaja straika Viktor Gyokeres kwenye orodha ya mastaa wanaofanya vizuri kwenye Ligi Kuu England msimu huu licha ya kuwapo kwa maneno mengi kuhusu ubora wa mshambuliaji huyo wa Arsenal.

Gyokeres, 27, alijiunga na Arsenal kwenye dirisha lililopita akitokea Sporting Lisbon amefunga mabao sita katika mechi 14.

Hata hivyo, maswali ni mengi kama kiwango cha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden kinaweza kuisaidia Arsenal kufikia malengo ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu baada ya kukaribia kufanya hivyo kwa misimu mitatu iliyopita chini ya kocha Mikel Arteta.

Mabao matatu kati ya manne aliyofunga Gyokeres kwenye Ligi Kuu England msimu huu, alifunga dhidi ya timu zinazopambana kutoshuka daraja Leeds United na Burnley huku wengine wakihoji ubora wa staa huyo. Lakini, Rooney anavutiwa na mchezaji huyo na kumweka kwenye kundi la Antoine Semenyo na Bryan Mbeumo, ambao ni washambuliaji wengine hatari sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Wakati alipoulizwa kuhusu kuchagua wachezaji watatu ambao anadhani wamefanya vizuri hadi sasa kwenye Ligi Kuu England msimu huu, gwiji huyo wa Manchester United aliiambia Amazon Prime: "Tatu bora, bila shaka ipo na Antoine Semenyo, nadhani amekuwa bora sana Bournemouth, akiendeleza kiwango bora cha soka lake tangu msimu uliopita.

"Nitamweka Bryan Mbeumo pia. Nadhani amekuwa vizuri sana Manchester United, baada ya kuwa na mwanzo mgumu kwenye klabu. Kwa sasa amekuwa vizuri sana.

"Watatu, bila shaka nitakwenda na Gyokeres. Arsenal ilikuwa ikililia namba 9 mpya kwa miaka kadhaa na sasa imempata. Utendaji wake kazi ni mkubwa amekuwa akisaidia uchezaji wa timu na amekuwa akifunga pia, hivyo hiyo ndio tatu bora yangu."