Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rooney: Alexander Isak ajilaumu mwenyewe

ROONEY Pict

Muktasari:

  • Isak amepitia kipindi kigumu tangu alipoondoka Newcastle United kwa mgomo ili kulazimisha kujiunga na mabingwa wa England, Liverpool kwa ada ya Pauni 125 milioni. Mshambuliaji huyo raia wa Sweden amesema anataka “kuandika historia na kushinda mataji” akiwa Anfield.

LIVERPOOL, ENGLAND: GWIJI, Wayne Rooney amesema hana huruma kwa straika Alexander Isak, akidai mchezaji huyo ndiye wa kujilaumu mwenyewe baada ya kushuhudia uhamisho wake wa kuvunja rekodi ya Uingereza kwenda Liverpool ukigeuka kuwa janga.

Isak amepitia kipindi kigumu tangu alipoondoka Newcastle United kwa mgomo ili kulazimisha kujiunga na mabingwa wa England, Liverpool kwa ada ya Pauni 125 milioni. Mshambuliaji huyo raia wa Sweden amesema anataka “kuandika historia na kushinda mataji” akiwa Anfield.

Hata hivyo, hadi sasa amejikuta akipambana kupata nafasi kikosi cha kocha Arne Slot. Isak ameanza michezo sita pekee ya ligi na amefunga mabao matatu katika mechi 16 alizocheza kwenye mashindano yote. Ili kuongeza matatizo, Isak ameshindwa kuwa fiti kikamilifu na kwa sasa yuko nje ya uwanja kutokana na kuvunjika kifundo cha mguu, jeraha ambalo limemuweka nje tangu Desemba mwaka jana.

Badala ya kumwonea huruma mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, Rooney anaamini uamuzi wa Isak kugomea mazoezi Newcastle United ili kulazimisha uhamisho kwenda Liverpool unaanza kumrudia.

Gwiji wa zamani wa England na Manchester United alimwambia The Wayne Rooney Show: “Nadhani ni kosa lake mwenyewe. Hakufanya mazoezi na Newcastle. Hakuna ubaya kuomba kuondoka Newcastle kwenda Liverpool kiakili, pengine wachezaji tisa kati ya 10 wa Newcastle wangefanya hivyo sasa.

"Lakini, namna alivyofanya jambo hilo, kwa kukataa kufanya mazoezi na timu, ilimwacha nyuma kwa kukosa maandalizi ya msimu. Ndipo akapata jeraha lake la kwanza. Najua jeraha la pili lilitokana na madhara ya faulo, lakini hajawahi kuwa tayari kimchezo tangu ajiunge na Liverpool, kwa maoni yangu. Mara nyingi tunazungumzia upande wa kisaikolojia wa mchezo na kuna presha kubwa unapocheza katika klabu kubwa.”