Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak kukaa nje siku kibao

ISAK Pict

Muktasari:

  • Staa huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni 130 milioni kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi alilazimika kutolewa kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham katika Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita.

LIVERPOOL, ENGLAND: STRAIKA wa Liverpool, Alexander Isak anakabiliwa na muda mrefu wa kuwa nje ya uwanja baada ya kuripotiwa kuwa na mpasuko kwenye mfupa wa mguu.

Staa huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni 130 milioni kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi alilazimika kutolewa kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham katika Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita.

Isak aligongana na beki wa Spurs, Micky van de Ven wakati alipokuwa akifunga bao la kwanza la Liverpool.

Akiwa ameingia kutokea benchini kuchukua nafasi ya Conor Bradley, Isak alifanikiwa kufunga bao lake la tatu la msimu.

Lakini, alibaki chini baada ya kufunga bao hilo na kuhitaji msaada wa madaktari wa Liverpool. Na baada ya hapo, straika huyo alihitaji vipimo vya MRI kutambua ukubwa wa tatizo lake na ni muda gani atakuwa nje ya uwanja.

Na Liverpool inajiandaa kumkosa mchezaji wao huyo iliyemsajili kwa pesa nyingi kwa muda mrefu. Hilo ni pigo kubwa kwa kocha Arne Slot, ambaye alitoa Pauni 130 milioni na kuvunja rekodi ya uhamisho huko Uingereza wakati ananasa saini yake akitokea Newcastle United kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

“Ngoja tusubiri tuone itakavyokuwa,” amesema Slot alipoulizwa kuhusu hali ya Isak.

Mohamed Salah hayupo kwenye kikosi cha Liverpool kwa sasa akitumikia Misri kwenye mashindano ya Afcon 2025, hivyo kocha Slot atabaki na huduma ya straika Hugo Ekitike, ambaye alisajiliwa na kwa Pauni 79 milioni kutoka Eintracht Frankfurt.