Isak haijulikani atarudi lini dimbani
Muktasari:
- Staa huyo usajili wa rekodi katika kikosi cha Liverpool aloijiumiza wakati anafunga bao la kwanza katika mechi hiyo.
LIVERPOOL, ENGLAND: STRAIKA Alexander Isak amefanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika mfupa wa mguu katika mechi dhidi ya Tottenham.
Staa huyo usajili wa rekodi katika kikosi cha Liverpool aloijiumiza wakati anafunga bao la kwanza katika mechi hiyo.
Isak, 26, alitolewa uwanjani baada ya kushindwa kuendelea na mechi ambayo Liverpool ilishinda 2-1.
Klabu yake sasa imetoa taarifa upasuaji umefanikiwa na mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu ili kuugusa jeraha hilo lilitokana na kupata mpasuko kwenye mfupa mdogo wa mguu.
Hata hivyo, kinachotia wasiwasi ni haifahamiki muda kamili ambao mshambuliaji huyo atakuwa nje ya uwanja.
Taarifa ya Liverpool ilibainisha: “Alexander Isak amefanyiwa upasuaji kutibu maumivu aliyopata Jumamosi. Straika huyo wa Liverpool alijiumiza wakati anafunga bao la kwanza dhidi ya Tottenham Hotspur na kulazimika kutolewa.
“Baada ya kufanyiwa vipimo, upasuaji umefanyika kwenye eneo la kifundo cha mguu kwa sababu alipata mpasuko wa mfupa mdogo wa mguu. Ataendelea kujiuguza kwenye uwanja wa mazoezi wa AXA Training Centre na haijulikani atarudi lini.”
Licha ya kwamba haijawekwa wazi atarudi lini uwanjani, lakini kuna imani kubwa Isak akacheza tena msimu huu.
Katika mchezo huo, bao jingine la Liverpool lilifungwa na Hugo Ekitike, wakati lile la kujifariji la Spurs lilifungwa na Richarlison kwenye dakika za mwisho. Isak alijiunga na Liverpool kwa ada ya Pauni 130 milioni kutokea Newcastle United dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.