Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo hatoki Saudia

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa kutoka Goal.Com, mkataba huo mpya atakaosaini fundi huyo kutoka Ureno utamwezesha kukaa Saudia hadi mwaka 2026 na atakuwa amefikisha zaidi ya miaka 40.

RIYADH, SAUDI ARABIA: STAA wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo inadaiwa ana mpango wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa muda mrefu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Goal.Com, mkataba huo mpya atakaosaini fundi huyo kutoka Ureno utamwezesha kukaa Saudia hadi mwaka 2026 na atakuwa amefikisha zaidi ya miaka 40.

Ronaldo ambaye ameshinda tuzo tano za Ballon d’Or, mbali ya umri kumtumpa mkono haonekani kushuka kiwango na msimu huu akiwa amecheza mechi 47 na kufunga mabao 48.

Staa huyu wa zamani wa Man United, atafikisha umri wa miaka 40, Februari 2025 na mkataba wake wa sasa utakuwa umemalizika.

Al-Nassr inataka kumsainisha Ronaldo mkataba mpya kutokana na mchango wake uwanjani pamoja na faida za nje ya uwanja walizopata mara baada ya fundi huyo kutua kwani kampuni nyingi zimeingia nao udhamini wa kutangaza bidhaa zao.

Ben Jacobs ambaye ni mwandishi wa habari kutoka talkSPORT alisema: “Mwaka 2025 utakuwa ni muhimu sana kwa Saudia, kwanza mkataba wa Ronaldo ndio utakuwa unamalizika ingawa nafahamu ataongeza mwingine kwa mwaka mmoja zaidi, pili watakuwa wanaingia tena mikataba ya haki ya matangazo ya televisheni.”

“Kama unavyoona ikiwa Ronaldo atabaki akaingia Salah na Bruno kupata tena ya haki kurusha matangazo ya televisheni itahitaji kutoa kiasi kikubwa sana cha pesa hali itakayowapa faida Saudia kwa sababu wachezaji hao wana ushawishi mkubwa na wataenda kufanya ligi itazamwe zaidi kimataifa.”

“Nimembiwa mabosi wa ligi hiyo wanataka mchezaji mwingine kutoka Ureno na nguvu zao wanataka kuziwekeza kwa Bruno.”