Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo amiliki timu Hispania

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Ronaldo, 41, bado anaendelea kufunga mabao mengi akiwa na Al-Nassr FC katika Ligi Kuu Saudia na atarejea kwenye jukwaa kubwa zaidi msimu huu wa joto katika fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada.

RIYADH, SAUDI ARABIA: SUPASTAA, Cristiano Ronaldo ameanza hatua zake za kwanza katika ulimwengu wa umiliki wa klabu za soka kwa kununua hisa asilimia 25 katika klabu ya Hispania, UD Almeria.

Ronaldo, 41, bado anaendelea kufunga mabao mengi akiwa na Al-Nassr FC katika Ligi Kuu Saudia na atarejea kwenye jukwaa kubwa zaidi msimu huu wa joto katika fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Hata hivyo, nahodha huyo wa Ureno tayari ana mipango ya maisha baada ya kustaafu soka. Hivi karibuni ilitangazwa Ronaldo amekuwa mmiliki mwenza wa Almeria, wanaocheza katika Daraja la Pili la soka nchini Hispania.

Ununuzi huo umefanywa kupitia kampuni ya CR7 Sports Investments, mwaka mmoja baada ya Almeria kuchukuliwa na kundi la uwekezaji kutoka Saudi Arabia. Katika taarifa yake, Ronaldo amesema: “Kwa muda mrefu nimekuwa na ndoto ya kuchangia soka nje ya uwanja wa michezo. UD Almeria ni klabu ya Hispania yenye misingi imara na uwezo mkubwa wa kukua. Natazamia kufanya kazi pamoja na uongozi wa klabu ili kusaidia hatua inayofuata ya maendeleo yake.”

Uwekezaji wake unaweza kuwa hatua ya kwanza kuelekea ndoto ya kumiliki klabu yake ya zamani, Manchester United. Klabu hiyo imepitia mabadiliko ya umiliki katika miaka miwili iliyopita, huku Jim Ratcliffe kupitia kampuni yake ya INEOS akinunua hisa ndogo na kuchukua udhibiti wa shughuli za soka za klabu.

Akizungumza katika hafla ya Dubai Globe Soccer Awards mwaka 2024, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or alizungumzia changamoto za Man United na kudokeza kuwa angeweza kurekebisha matatizo yao iwapo angekuwa mmiliki wa klabu hiyo.

“Tatizo la Manchester United ni lilelile,” amesema Ronaldo na kuongeza. “Tatizo si kocha kila wakati. Ni zaidi ya hapo. Kama ningekuwa mmiliki wa klabu, ningeweka mambo wazi na kurekebisha yale ambayo hayako sawa.”