Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Robinho sasa kufungwa Brazil

Muktasari:

  • Robinho ambaye sasa ana umri wa miaka 40, atakamatwa huko Santos ambako anaishi.

Sao Paulo, Brazil. Mchezaji wa zamani wa Manchester City, Robinho atatumikia kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya unyanyasaji wa kijinsi na mahakama ya juu huko nchini Brazil.

Robinho alifanya kosa hili huko nchini Italia ambako alihukumiwa kifungo cha miaka tisa jela na mahakama za nchi hiyo zilitoa kibali cha kukamatwa kwake kama angetoka nje ya Brazil, lakini staa huyu aliendelea kula bata kule jijini Sao Paulo na hakutoka kabisa nje ya nchi hiyo.

Hiyo ilisababisha mamlaka nchini Italia kutuma maombi Brazil ili staa huyo akamatwe na kutumikia adhabu kwa makosa hayo aliyofanya mwaka 2017, ambayo yeye mwenyewe anadai hakuyafanya.

Kutokana na ombi hilo, mahakama ya juu ya haki nchini Brazil ilikaa kikao na kupiga kura ambapo wajumbe tisa kati ya 15 walipitisha suala la mchezaji huyo kutumikia kifungo chake nchini Brazil.

Kikao hicho hakikujadili wala kupitia kesi kujua kama Robinho amefanya kosa hilo kweli au laa, badala yake uamuzi huo unamfanya staa huyu kukamatwa na kutumikia kifungo hicho mara moja.

Robinho anadaiwa kuwa mmoja kati ya wanaume sita waliomfanyia unyanyasaji wa kijinsi mwanamke mmoja raia wa Albania kwenye ukumbi wa starehe nchini Italia, Januari 22, 2013 wakati anaichezea AC Milan.

Alikutwa na hatia Novemba, 2017 na mahakama nchini Italia na baada ya hapo alikata rufaa mara kadhaa lakini bado alikutwa na hatia.

Hata hivyo, katiba ya Brazil hairuhusu raia wa nchi hiyo aliyehukumiwa nje ya nchi kutumikia kifungo chake Brazil ingawa inaweza kutokea kutokana kwa utaratibu maalumu kama ilivyofanyika kwa Robinho.

Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na AC Milan ambaye sasa ana umri wa miaka 40, atakamatwa huko Santos ambako anaishi.

Aliwahi kukiri kwamba aliwahi kuwa kwenye mawasiliano na mwanamke aliyedaiwa kumfanyia unyanyasaji wa kijinsi lakini alidai ilikuwa ni kwa makubaliano.