Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riccardo Calafiori kuikabili Spurs Jumapili

CALAFIORI Pict

Muktasari:

  • Wachezaji ambao wapo kwenye mashaka ya kucheza mechi dhidi ya Spurs ni beki Gabriel Magalhães anayekabiliwa na majeraha ya misuli ya paja kama ilivyo kwa Viktor Gyökeres, huku Kai Havertz akipona jeraha ambalo limekuwa likimuweka nje kwa muda.

Beki wa kushoto wa Italia, Riccardo Calafiori, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu ya EPL dhidi ya Tottenham Hotspur itakayopigwa Jumapili, Novemba 23, 2025 kwenye Uwanja wa Tottenham.

Hii huenda ikawa habari njema kwa Arsenal hasa kufuatia taarifa za kuumia kwa Gabriel Magalhaes, ambaye sasa kuna shaka kubwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha The Gunners kwenye mechi hiyo ya North London Derby, baada ya kumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Brazil iliyocheza dhidi ya Senegal, Jumamosi iliyopita, Novemba 15, 2025.

Calafiori aliibua hofu kubwa, baada ya kuondolewa kwenye kikosi cha Italia, kufuatia majeraha ya paja, lakini kwa haraka madaktari wa Arsenal walianza kumfanyia matibabu.

Hata hivyo, The Daily Cannon imeripoti kuwa, Calafiori yupo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumapili dhidi ya Spurs inayoshika nafasi ya sita, kwa kufikisha pointi 17 katika msimamo wa Ligi Kuu ya EPL.

CALA 01

Calafiori aliyesajiliwa Arsenal mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Bologna ya Italia kwa ada ya Pauni 42 milioni, ameshacheza mechi 17 za michuano yote msimu huu, akianza katika mechi 12.

Wachezaji ambao wapo kwenye mashaka ya kucheza mechi dhidi ya Spurs ni beki Gabriel Magalhães anayekabiliwa na majeraha ya misuli ya paja kama ilivyo kwa Viktor Gyökeres, huku Kai Havertz akipona jeraha ambalo limekuwa likimuweka nje kwa muda.

Mwingine ni Martin Ødegaard, ambaye anaendelea kupona jeraha la goti. Pia Noni Madueke na Gabriel Martinelli wote hawatakuwepo kutokana na jeraha la misuli na goti.