Rekodi hizi zinaishi

Muktasari:

  • Mbali ya ubingwa, kwa msimu huu pia kuna rekodi mbalimbali zilizowekwa tangu kuanza kwa msimu huu na iliyopita. Leo tunakuleta baadhi ya rekodi kubwa ambazo ziliwekwa kwenye nyakati mbalimbali na hadi leo hazijafutwa.

PARIS, UFARANSA: Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1)  inaelekea ukingoni, PSG ndio inapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu ambapo litakuwa taji la 12.


Mbali ya ubingwa, kwa msimu huu pia kuna rekodi mbalimbali zilizowekwa tangu kuanza kwa msimu huu na iliyopita. Leo tunakuleta baadhi ya rekodi kubwa ambazo ziliwekwa kwenye nyakati mbalimbali na hadi leo hazijafutwa.

MATAJI
Paris Saint-Germain ndio inayoshika rekodi ya kuwa na mataji mengi (11), Lyon ndio timu iliyochukua mataji mengi mfulilizo (7) kuanzia msimu wa 2002-2008. Pia  Paris Saint-Germain hadi sasa ndio timu iliyomaliza msimu kwa pointi nyingi tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2015 -16 ilipochukua pointi 96.

USHINDI MECHI NYINGI 
Paris Saint-Germain (2015-16) na Monaco (2016-17), zilishinda mechi 30 kwenye mechi 38.


Saint-Etienne (1969- 70) ilishinda mechi 25 katika michezo 34.
Ushindi mechi nyingi nyumbani: Saint-Etienne, mechi (1974 -75)
Ushindi mechi nyingi ugenini: Paris Saint-Germain mechi 15 msimu wa (2015-16)


Ushindi mechi nyingi mfululizo: Paris Saint-Germain, mechi 14 msimu wa (2018-19)


Ushindi mechi nyingi nyumbani mfululizo: Saint-Etienne, mechi  28 kati ya Machi 13, 1974 na Agosti, 27, 1975.


Ushindi  mechi nyingi ugenini mfululizo: Marseille, mechi tisa kati ya Februari 15,  2009 na Agosti, 19, 2009.


Ushindi mkubwa zaidi: Sochaux 12-1 Valenciennes     (Julai, 1935).


Ushindi mkubwa ugenini: Troyes 0-9 Paris Saint-Germain (Machi 13, 2016)


Unbeaten ndani ya msimu mmoja: Nantes mechi 32, msimu wa 1994- 95.


Unbeaten mechi za nyumbani: Nantes (kati ya Mei, 15, 1976 hadi April, 07, 1981)


Unbeaten kiujumla: Paris Saint-Germain mechi 36 kati ya Machi 15, 2015 na Februari 20, 2016.


Kupoteza mechi chache nyumbani msimu mmoja: Nantes, mechi moja msimu wa 1994-95.


Kupoteza mechi chache ugenini msimu mmoja: Sochaux (1934-35), Saint-Etienne (1969-70), Nantes (1994-95), Marseille (2008-09) na Paris Saint-Germain (2015-16), zote zilipoteza mechi moja.

MABAO
Kufunga mabao mengi msimu mmoja: RC Paris mabao 118 kwenye mechi 38 msimu wa 1959-60.
Lille, mabao 102 msimu wa 1948-49.


Kuruhusu mabao machache msimu mmoja: Paris Saint-Germain, mabao 19 msimu wa 2015-16.


Kuruhusu mabao machache ya nyumbani kwa msimu mmoja: Saint-Etienne, mabao manne msimu wa (2007-08)

Kuruhusu mabao machache ugenini msimu mmoja: Paris Saint-Germain, mabao saba msimu wa 2015-16).

NIDHAMU
Msimu uliokuwa na kadi nyingi za njano:  2002-03 kadi 654
Timu iliyopata kadi nyingi nyekundu msimu mmoja: Montpellier kadi 14 msimu wa 2013-14.

MAHUDHURIO
Msimu uliokuwa na mahudhurio makubwa viwanjani: 
2018/19 watu  8,676,490.


Mechi iliyohudhuriwa na  mashabiki wengi: Lille vs Lyon, kwenye uwanja wa  Stade de France ambayo ilihudhuriwa na  mashabiki  78,056, Machi 07,  2009.