Refa wa gemu ya Man United na Palace kuvaa kamera kichwani

Muktasari:

  • Mwamuzi, Jarred Gillet atavaa kichwani kifaa hicho kinachofahamika kama ‘RefCam’, ambapo itakuwa mara ya kwanza kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND:  Kwa mara ya kwanza, mwamuzi atakayechezesha mchezo wa Ligi Kuu England baina ya Crystal Palace na Manchester United utakaofanyika usiku wa leo huko Selhurst Park atavaa kamera kichwani.

Mwamuzi, Jarred Gillet atavaa kichwani kifaa hicho kinachofahamika kama ‘RefCam’, ambapo itakuwa mara ya kwanza kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

Kifaa hicho kitakuwa kinarekodi mechi hiyo, lakini picha zake hazitarushwa mubashara.

Na badala yake, picha ambazo zitapigwa na kamera hiyo zitatumika kwenye kipindi cha Mic'd Up kinachohusu waamuzi.

Kipindi hicho kinarushwa na televisheni ya Sky Sports kinahusu uchambuzi wa kilichofanywa na waamuzi kwenye mechi, kikimhusisha pia bosi wa PGMOL, Howard Webb, ambaye hivi karibuni alikiri kwamba Nottingham Forest walistahili penalti kwenye mechi dhidi ya Everton mwezi uliopita. Kamera hiyo imethibitishwa na kupitishwa na IFAB, Ligi Kuu England, PGMOL na klabu zote mbili zitakazohusika kwenye mechi ya majaribio. Wachezaji wote wanafahamishwa kuhusu kamera hiyo, hivyo wataonywa na makocha wao juu ya kumzonga mwamuzi na kutoa matamshi mabaya, yatarekodiwa.

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes amekuwa maarufu kwa kuwazonga na kuwasemesha waamuzi, hivyo kamera hiyo inaweza kuwa mtego wa kumweka kwenye hatia.

Gillett aliwahi kutumika kwenye mechi ya majaribio ya aina hiyo katika mchezo wa A-League kati ya Sydney FC na Melbourne City huko Australia. imba 45 za kwanza dhidi ya Tabora United