Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usyk ndiye mbabe, Fury apinga matokeo

Muktasari:

  • Pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu, hatimaye lilishuhudiwa Usky akimchapa Fury kwa pointi za majaji, kitendo kilichofuatia kwa Fury kudai yeye ndiye mshindi.

RIYADH, SAUDI ARABIA: Jana Jumamosi usiku, Jiji la Riyadh, Saudi Arabia na dunia zilisimama kwa muda kuipisha miamba miwili ya masumbwi ya uzito wa juu Tyson Fury dhidi ya Oleksandr Usyk, kwenye Ukumbi wa Kingdom Arena.

Pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu, hatimaye lilishuhudiwa Usky akimchapa Fury kwa pointi za majaji, kitendo kilichofuatia kwa Fury kudai yeye ndiye mshindi.


KURA ZILIVYOKUWA

Baada ya raundi 12, pointi za majaji ndio ziliamua na jaji wa kwanza alitoa pointi 115-112, wa pili 114 -113 na wa tatu 114-113.

Matokeo hayo yalimpa ubingwa Usyk na kumfanya Fury, 35, apoteze kwa mara ya kwanza katika miaka 16 aliyodumu kwenye mchezo wa ndondi na hivyo, Usyk kupata mkanda wake wa nne wa uzito wa  juu wa dunia.


FURY ACHARUKA

Licha ya kupoteza pambano hilo, bondia huyo Mwingireza amesema yeye ndio alishinda raundi nyingi kuliko mpinzani wake na anaamini watu wamepanga matokeo.

"Naamini alishinda raundi chache, namimi nilishinda raundi nyingi, najua pengine ni kwa sababu nchi yake ipo katika vita, kwa hiyo watu wameegemea upande wake zaidi, lakini wangefanya uamuzi kiusahihi kabisa kwa maoni yangu, mimi ndio nimeshinda," alisema Fury.

"Ni moja kati ya matokeo ya kupangwa zaidi kuwahi kutokea katika mchezo wa ngumi, lakini bado nitakutana naye tena."


USKY MBABE

Kabla ya  kuchukua mkanda huo wa WBC kutoka kwa Fury, Usyk alikuwa akimiliki mikanda mingine kama WBA, WBO na IBF.

Wakati rekodi ya Fury ya kutokupigwa ikivunjwa, Usky ameendelea kushikilia rekodi yake ya kutopoteza pambano lolote ndani ya miaka 25 ya upambanaji wake.

Baada ya pambano hilo, amesema:"Nawashukuru sana watu wangu, pamoja n timu yangu, ushindi huu ni furaha kubwa kwangu, familia yangu na nchi yangu, pia nipo tayari kwa mechi ya marudiano."