Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Redknapp ampiga kijembe Gyokeres

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Kwa Gyokeres baada ya kufunga mkwaju wake wa penalti alionekana kuvutiwa na jambo hilo na kusema ni kitu kizuri kwa sababu imeiwezesha Arsenal kupata ushindi.

LONDON, ENGLAND: STAA wa zamani wa Ligi Kuu England, Jamie Redknapp amempiga kijembe straika wa Arsenal, Viktor Gyokeres akidai kwamba hana uwezo wa kucheza kwenye kikosi cha The Gunners licha ya kwamba alisajiliwa kwa pesa nyingi.

Staa huyo wa zamani wa Tottenham na Liverpool hakushawishika na kiwango cha Gyokeres katika mechi dhidi ya Everton licha ya kwamba alifunga bao pekee katika mechi hiyo kwa mkwaju wa penalti.

Gyokeres alifunga penalti na kuipa Arsenal pointi tatu muhimu zilizowarudisha kwenye kilele cha msimu wa ligi. Hilo lilikuwa bao la tano kwenye Ligi Kuu England katika msimu huu, lakini likiwa na kwanza tangu Novemba 1.

Dhidi ya Everton, Gyokeres alichukua majukumu ya kupiga penalti kutoka kwa Bukayo Saka na kufanikiwa kufunga, lakini Redknapp amekuwa na mawazo tofauti juu ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Sporting CP.

"Anajaribu kufanya vizuri, lakini yupo kwenye wakati mgumu kwa kipindi hiki," amesema Redknapp.

"Ni bao la tatu kwa msimu, kwa vyovyote itakavyoelezwa, lakini alikuwapo kwenye ligi ya England huko nyuma, hivyo nashangaa kuona anateseka kwa sasa. Ukitazama mwili wake ulivyo, ungedhani angekuwa tishio kwenye matumizi ya nguvu, lakini hana huo uwezo."

Kwa Gyokeres baada ya kufunga mkwaju wake wa penalti alionekana kuvutiwa na jambo hilo na kusema ni kitu kizuri kwa sababu imeiwezesha Arsenal kupata ushindi.