Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta: Gyokeres? Wenzake ndo shida

Muktasari:

  • Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves, Jumamosi iliyopita, huku mabao yote matatu yaliyofungwa katika mechi hiyo yakipatikana katika dakika 20 za mwisho huku lile la ushindi likiwa kwenye dakika za majeruhi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amemtetea straika Viktor Gyokeres kwa kiwango chake alichokionyesha dhidi ya Wolves na badala yake amewaangushia mzigo mastaa wenzake katika kikosi hicho cha Emirates.

Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves, Jumamosi iliyopita, huku mabao yote matatu yaliyofungwa katika mechi hiyo yakipatikana katika dakika 20 za mwisho huku lile la ushindi likiwa kwenye dakika za majeruhi.

Bao la kujifunga la Sam Johnstone kutokana na mpira wa kona wa Bukayo Saka iliifanya Arsenal kuongoza kabla ya Tolu Arokodare kuisawazishia Wolves. Na kama zali kwa Arsenal, Yerson Mosquera kwa bahati mbaya alipiga kichwa na kuutumbukiza mpira kwenye nyavu zake katika dakika za majeruhi na hivyo kuisaidia Arsenal kuzoa pointi zote tatu.

Ikikabiliana na timu inayoburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, Arsenal ilishindwa kabisa kuonyesha ubora wake, huku kocha Arteta akitoa sababu za ugumu huo waliokabiliana nao.

Alisema: “Tulifahamu wazi ingekuwa mechi ngumu, hasa unaposhindwa kupata bao mapema. Tulikuwa na mambo mengi kwenye kipindi cha kwanza, nafasi moja kubwa kabisa ya Martinelli, alikuwa mita mbili tu (jirani na lango) na hakukabwa, lakini alishindwa kufunga.

“Lakini, tulishindwa kufanya vizuri kwenye maeneo ya hatari. Tulikabiliana na vitu vingi na baadaye tulishindwa kutengeneza nafasi za wazi. Kwenye kipindi cha pili, tulikuwa vizuri na tulifunga bao. Wao mara moja tu waliyotushambulia, walifunga. Hivyo ndivyo Ligi Kuu England ilivyo.”

Wolves ilicheza kwa kukabia chini katika mechi hiyo ya Emirates na hivyo kumfanya Gyokeres kukosa nafasi ya kushambulia. Katika mechi hiyo, Gyokeres aligusa mpira mara 15 tu kwa dakika 81 alizocheza, lakini Arteta aliwashutumu wachezaji wenzake kwamba hawakumpa ushirikiano wa kutosha.