Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid ikimvutia waya Klopp, wanambeba

KLOPP Pict

Muktasari:

  • Real Madrid ilitangaza kumfuta kazi Xabi Alonso, Jumatatu iliyopita, ambapo Mhispaniola huyo alimaliza kipindi cha misukosuko baada ya kupoteza katika fainali ya Super Cup ya Hispania mbele ya mahasimu wao wakubwa, Barcelona.

MADRID, HISPANIA: JURGEN Klopp ametajwa kuwa kinara kwenye orodha ya makocha wanaopewa nafasi ya kupewa kibarua Real Madrid huku ripoti zikifichua gwiji huyo wa Liverpool yupo tayari kukubali kazi hiyo.

Real Madrid ilitangaza kumfuta kazi Xabi Alonso, Jumatatu iliyopita, ambapo Mhispaniola huyo alimaliza kipindi cha misukosuko baada ya kupoteza katika fainali ya Super Cup ya Hispania mbele ya mahasimu wao wakubwa, Barcelona.

Kocha wa timu ya akiba ya Real Madrid, Alvaro Arbeloa, ameteuliwa kuchukua nafasi ya Alonso. Hata hivyo, bado haijabainika kama beki huyo wa zamani wa Liverpool na West Ham yupo kama kocha wa mpito au amekuwa kocha wa kudumu wa kikosi hicho cha Bernabeu.

Wazo la kwamba Los Blancos wanaweza kufanya uteuzi mwingine ili kuokoa msimu wao bado halijatupiliwa mbali. Kwa sasa Real Madrid ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga, pointi nne nyuma ya Barcelona.

Klopp, mwenye umri wa miaka 58, ameibuka kama mmoja wa wanaowania nafasi hiyo iwapo itakuwa wazi, na Sky Sports inaripoti kuwa endapo mabingwa hao Ulaya mara 15 wangemfuata, angezingatia hilo kwa umakini mkubwa. Mjerumani huyo kwa sasa ni mkuu wa soka la kimataifa wa kampuni ya Red Bull na ana mkataba wa muda mrefu, lakini wazo la kukaa kwenye kiti cha kocha wa Bernabeu linasemekana kumvutia sana.

Muda mfupi baada ya kuthibitishwa kufukuzwa kwa Alonso, Klopp alionekana kama mchambuzi wa michezo kwenye kituo cha Austria, ServusTV On, na kutoa maoni yake kuhusu hali ilivyo Madrid kwa ujumbe kwa viongozi wa klabu. “Simu yangu kwa kweli imekuwa ikiita ingawa si kutoka Madrid,” amesema Klopp na kuongeza:

“Lakini ndiyo, kulikuwa na watu waliodhani wanapaswa kuwasiliana nami moja kwa moja kuhusu hilo!

“Kwanza kabisa, nafikiri ni ishara nyingine kwamba mambo hayako sawa kabisa pale kwa sasa. Kama Xabi Alonso, ambaye kwa miaka miwili iliyopita Leverkusen alionyesha ana kipaji kikubwa cha ukocha nadhani kwa umri wake na idadi ya kazi alizofanya, hilo linaweza kusemwa wazi akilazimika kuondoka Madrid miezi sita tu baadaye, inaonyesha mambo kadhaa.”

Tangu aondoke Liverpool 2024, Klopp hajarejea kufundisha. Oktoba mwaka jana amesema soka la England huko ameshamaliza baada ya kuinoa Liverpool.