Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford hataki kurudi tena Manchester United

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Ripoti zimefichua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England yupo tayari kupunguza mshahara wake ili aendele kubaki Hispania na kuichezea Barclelona.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford, 28, inadaiwa hataki kurejea Manchester United pale mkataba wake wa mkopo Barcelona utakapomalizika mwisho wa msimu huu.

Ripoti zimefichua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England yupo tayari kupunguza mshahara wake ili aendele kubaki Hispania na kuichezea Barclelona.

Rashford inadaiwa kufurahia maisha na mfumo wa uchezaji wa Barcelona, jambo lililomfanya kufikia uamuzi huo, licha ya kocha mpya Michael Carrick kumhakikishia akipewa mkataba wa kudumu yupo tayari kumrudisha na kumfanya kuwa mchezaji tegemeo.

Hata hivyo, licha ya kuwa tayari kubaki katika viunga vya Nou Camp, uamuzi wa mwisho juu ya hatma yake utategemea sana na makubaliano kati ya mabosi wa Barca na Man United, juu ya masuala ya ada ya uhamisho.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2028, na msimu huu akiwa na Barca amecheza mechi 32 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 12.


Dayot Upamecano

BEKI wa kati wa Bayern Munich, Mfaransa Dayot Upamecano, 27, yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo. Upamecano amekuwa mhimili muhimu katika beki ya Bayern licha ya changamoto za majeraha.

Uongozi wa Bayern umeonyesha imani kubwa kwake kama sehemu ya mipango yao ya muda mrefu. Awali ilielezwa fundi huyu huenda akatimkia Real Madrid au Liverpool ambazo zilikuwa zinahitaji kumsajili dirisha lililopita.


Tyrell Malacia

BEKI wa kushoto wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Tyrell Malacia, 26, anaripotiwa kukasirishwa na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Jason Wilcox, baada ya kuzuia dili la yeye kuondoka Old Trafford siku ya mwisho ya dirisha la usajili.

Inaelezwa Malacia alikuwa tayari amepanda ndege kuelekea Uturuki kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Besiktas, kabla Wilcox kumjulisha kuwa lazima abaki Manchester United.


Raheem Sterling

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Chelsea, Raheem Sterling, 31, alikuwa katika mazungumzo na klabu ya Bundesliga, Union Berlin, katika siku za hivi karibuni.

Hata hivyo, klabu hiyo ya Ujerumani ilichagua kutomsajili, hivyo kumfanya Sterling kuendelea kusubiri hatima ya mustakabali wake.

Sterling anaendelea kutafuta changamoto mpya baada ya kuachana na Chelsea kabla ya dirisha lililopita kufungwa.


Karim Benzema

STRAIKA wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema, 38, yupo mbioni kuondoka Al-Ittihad na kujiunga na wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia, Al-Hilal.

Benzema alijiunga na Al-Ittihad katika dirisha la majira ya kiangazi ya mwaka 2023 akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu.

Uamuzi wa kuondoka unatajwa kuchochewa na mabadiliko ya mipango ya kiufundi Al-Ittihad pamoja na ofa aliyowekewa mezani.


Maghnes Akliouche

TOTTENHAM ilishindwa kukamilisha dili la kumsajili kiungo wa Monaco na timu ya taifa ya Ufaransa, Maghnes Akliouche, 23, katika dakika za mwisho za  dirisha lililopita la usajili.

Hata hivyo, Spurs bado haijakata tamaa na inatarajia kurejea tena mezani kwa ajili ya mchezaji huyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Akliouche amekuwa akionyesha kiwango bora Ligue 1, jambo linalomfanya kuendelea kuivutia Spurs.

Monaco inatarajiwa kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kumwachia mwisho wa msimu huu.


Lassine Sinayoko

WOLVES bado inatamani kumsajili mshambuliaji wa Auxerre, Lassine Sinayoko, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kufeli kukamilisha dili lake dirisha hili.

Kwa mujibu wa Football Insider, Wolves imevutiwa sana na kiwango ambacho fundi huyu amekionyesha katika michuano ya AFCON. Alikuwa ikihitajika pia na klabu za Championship, Coventry City na Middlesbrough.


Ibrahim Mbaye

LICHA ya dirisha la usajili kufungwa, Chelsea na Aston Villa zinamfuatilia kwa karibu  winga chipukizi wa Paris St-Germain, Msenegal Ibrahim Mbaye, 18.

Hata hivyo, PSG inamwona kinda huyu kama mradi wa baadaye, lakini presha kutoka klabu za Ligi Kuu England inaweza kuwalazimu kufikiria hatma yake ikiwa ni kumuongeza mkataba mpya au kumtoa kwa mkopo kwenda timu itakayompa nafasi zaidi ya kucheza.