Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford bado ana jambo Nou Camp

Rashford Pict

Muktasari:

  • Rashford alijiunga na Villa kwa mkopo wa nusu msimu dirisha lililopita la majira ya baridi ili kutafuta nafasi ya kucheza baada ya kuondolewa katika kikosi cha Man United.

BARCELONA, HISPANIA: MSHAMBULIAJI wa Manchester United anayecheza kwa mkopo Aston Villa, bado hajakata tamaa kuhusu ndoto yake ya kuhamia Barcelona licha ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Deco, kusema wiki hii vigogo hao hawakuwa “na shinikizo” la kumsajili dirisha lililopita.

Rashford alijiunga na Villa kwa mkopo wa nusu msimu dirisha lililopita la majira ya baridi ili kutafuta nafasi ya kucheza baada ya kuondolewa katika kikosi cha Man United.

Mchezaji huyo, 27, aliweka wazi yupo tayari kwa ajili ya changamoto mpya nje ya mashetani hao wekundu baada ya kuachwa na Amorim  kikosi cha timu hiyo kilichocheza dabi dhidi ya Manchester City, Desemba mwaka jana.

Ndugu zake ambao wanafanya kazi kama mawakala wake walifanya mazungumzo na timu kadhaa za Ulaya, ikiwemo Barcelona.

Hata hivyo,  Barca haikuwekeza nguvu sana ya kumsajili hali iliyosababisha atue Villa.

Deco alisema: “Ni kweli kulikuwa na mazungumzo kuhusu Rashford, lakini hatukujitahidi sana kuhakikisha anakuja.”

Katika mahojiano yake baada ya kujiunga na Villa, Rashford alisema alikuwa na furaha kuhusu fursa ya kucheza tena soka.

Pia alieleza wazi hakujiona akiwa na muda mrefu wa kudumu  kwenye timu hiyo licha ya mkataba wake wa mkopo kuwa na kipengele kinachowapa Villa nguvu ya kumnunua mwisho wa msimu kwa Pauni 40 milioni.

Chanzo kililiambia tovuti ya The Sun bado staa huyu anana matumaini ya kuhamia Nou Camp.

“Marcus ana imani ikiwa atarejesha kiwango chake akiwa na Villa na kwa kuanza kufunga mabao, Barcelona watafufua nia ya kutaka kumsajili tena, hivyo ana motisha sana ya kutaka kufanya vizuri jambo ambalo ni zuri kwa Villa.”