Rashford avunja rekodi ya Ronaldo

New Content Item (3)
New Content Item (3)

MANCHESTER, ENGLAND. MARCUS Rashford amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao lake ya 25 kwenye mashindano ya Ulaya katika historia ya klabu, Manchester United ikitinga robo fainali ya Ligi ya Europa.

Rashford aliisaidia timu yake kutinga hatua hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Real Betis, katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 bora mashetani wekundu waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 uwanja wa Old Trafford.

Mbali na rekodi hiyo Rashford alifunga bao la 27 msimu huu, mabao 19 alifunga katika mechi 24 alizocheza tangu aliporejea baada ya fainali za Kombe la Dunia yaliyomalizika Qatar.
Mashabiki wa Man United walimsifia Rashford baada ya kuvunja rekodi ya Ronaldo ambaye alifunga mabao 24 baada ya kurejea Man United akitokea Juventus.

Mashabiki hao walimuandikia Rashford salamu za pongezi kupitia akaunti za Twitter, wengi wakidai straika huyo alijifunza mengi kutoka kwa Ronaldo ambaye sasa anakipiga Al-Nassr.

Mabao mawili ya Ronaldo kati ya matatu aliyoifungia Man United yalipatikana katika Ligi ya Europa dhidi ya timu kutoka Maldova, Sheriff Tiraspol. Ronaldo alifunga bao kwa mkwaju wa penalti ugenini kabla ya kufunga bao lingine uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa marudiano. Bao hili lilikuwa la mwisho kwake akiwa na uzi wa masheteni wekundu.

Naye Erik ten Hag alimsifia Rashford baada ya kumpiku Ronaldo kwenye orodha ya wachezaji wa Man United wanaoongoza kwa kucheka na nyavu kwenye michuano ya Ukaya.

"Timu ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga, Rashford alipata nafasi pia lakini nyingine akapoteza, hata hivyo akapambana na akafanikiwa kufunga, alistahili kutokana na jitihada alizoonyesha kwenye mechi dhidi ya Sporting Lisbon, straika mzuri anafahamu jinsi ya kuzitumia nafasi, huwezi kupoteza nafasi zaidi ya tano lazima katika hizo mbili au tatu zitaingia tu kwenye nyavu," alisema Ten Hag.