Jamie Carragher ashangaa Trent kuzomewa

Muktasari:
- Trent, ambaye ni zao la akademia ya klabu ya Liverpool alijikuta kwenye wakati mgumu na kuandamwa na mashabiki kwenye mechi hiyo baada ya kufahamika mwisho wa msimu atatimkia zake Real Madrid.
LIVERPOOL, ENGLAND: GWIJI wa Liverpool, Jamie Carragher amekiri kushangazwa kwa kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kumzoea Trent Alexander-Arnold kwenye mchezo dhidi ya Arsenal uliofanyika uwanjani Anfield, Jumapili.
Trent, ambaye ni zao la akademia ya klabu ya Liverpool alijikuta kwenye wakati mgumu na kuandamwa na mashabiki kwenye mechi hiyo baada ya kufahamika mwisho wa msimu atatimkia zake Real Madrid.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 2-2, Trent alianzia benchi ili kutoka nafasi kwa Conor Bradley. Alianza kuzomewa wakati alipokuwa akijiandaa kuingia uwanjani na mashabiki hao waliendelea kufanya hivyo kila alipogusa mpira.
Alipoulizwa juu ya maoni yake baada ya mechi, staa huyo wa zamani wa Liverpool, Carragher alidai kushangaza na idadi ya mashabiki waliokuwa wakimzomea Trent na kusema hakubaliani nao. Lakini, baadaye alisema anawaelewa kwani hawakufurahia uamuzi wa Trent.
Carragher alisema: “Hiyo ndiyo stori ya mchezo huo kuzomea. Sasa ndicho tunachokizungumzia na kitaripotiwa kwenye magazeti yote. Kilichonishangaza ni idadi ya mashabiki. Unapokuwa na watu 60,000, bila shaka kuna ambao hawakuwa na furaha na Liverpool na hali ilivyo, hilo linaeleweka.
Beki huyo wa zamani wa Liverpool alisema kiuhalisia hakuna mchezaji yeyote kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Anfield kwa sasa ambaye atakuwa hataki kwenda Real Madrid.