Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford aingia katika anga za PSG, AC Milan

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Rashford kwa sasa yupo kwa mkopo Barcelona, lakini klabu hizo ziko tayari kuingilia kati iwapo Barca haitakamilisha uhamisho wa kudumu wa mchezaji huyo.

PSG na AC Milan zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya straika wa Manchester United, Marcus Rashford, 28, na zinaweza kutuma ofa ya kumsajili katika dirisha lijalo.

Rashford kwa sasa yupo kwa mkopo Barcelona, lakini klabu hizo ziko tayari kuingilia kati iwapo Barca haitakamilisha uhamisho wa kudumu wa mchezaji huyo.

Klabu hizo zimeanza kuinyemelea saini ya Rashfrod baada ya kuona Barca ambayo ina kipengele cha kumnunua mazima kwa Pauni 26 milioni inasuasua kukamilisha dili kutokana na changamoto za kifedha.

Mara kadhaa Barca Camp wamekuwa wakiomba kupunguziwa bei ili kufanikisha mchakato huo, lakini Man United imegoma.

Mbali ya kuomba kupunguziwa bei, Barca pia imejaribu kuomba kupewa Rashford kwa mkopo wa msimu mmoja zaidi, lakini Man United imekataa. Mkataba wa nyota huyo unatarajiwa kumalizika 2028 na ameonyesha kiwango bora msimu huu.


Michael Olise

BAYERN Munich imekanusha taarifa zinazodai kuwa itamruhusu winga wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise mwenye umri wa miaka 24, kujiunga na Liverpool katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa kuwa hata kama Liverpool itatoa ofa kubwa inayozidi Pauni 170 milioni, Bayern haina mpango wa kumuachia nyota huyo. Mabosi wa Bayern wanaamini Olise ni sehemu muhimu ya uti wa mgongo wa timu yao kwa sasa.


Sandro Tonali

MANCHESTER United imepanga kufanya mawasiliano na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Italia, Sandro Tonali, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa kuwa Man United itawasilisha ofa yao mwishoni mwa msimu, inayoweza kufikia Pauni 70 milioni na ipo tayari kumpa mshahara wa takribani Pauni 250,000 kwa wiki. Hata hivyo, Newcastle inaweza kugomea dili lolote la kumuachia nyota huyo.


Myles Lewis-Skelly


MANCHESTER United imeongeza jina la beki wa kushoto wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly, 19, kwenye orodha ya wachezaji inaotaka kuwasajili dirisha lijalo la  majira ya kiangazi.

Inaelezwa nyota huyo ameomba kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Arsenal, hali inayoweza kufungua mlango wa kuondoka kwake. Man Utd inaonekana kuvutiwa naye.


Julian Alvarez

ARSENAL  imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Arsenal inataka kuongeza nguvu katika safu  ya ushambuliaji, na Alvarez anaonekana kuwa chaguo sahihi kutokana na uwezo wake wa kufunga na kucheza katika nafasi mbalimbali. Alvarez mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2030.


Ferran Torres

AATLETICO Madrid imeweka wazi nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa Atletico inataka kuimarisha safu ya ushambuliaji, na Torres anaonekana kuwa chaguo lao namba moja kutokana na uzoefu wake katika La Liga.

Kwa sasa fundi huyu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Barca na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027. Msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote na kufunga mabao 16.


Ben White

NEWCASTLE United inamwangalia beki wa Arsenal, Ben White, 28, kama mmoja kati ya mastaa inaotaka kuwasajili ili kuziba pengo la Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 35.

Inaelezwa kuwa Newcastle inaangalia uwezekano wa kufanya mabadiliko katika safu ya ulinzi, huku White akionekana kuwa chaguo bora kutokana na uzoefu wake wa kucheza katika nafasi zaidi ya moja.


Iliman Ndiaye

LIVERPOOL ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal, Iliman Ndiaye, 26, kutoka kwa mahasimu wao wa jiji, Everton katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mbali ya Liverpool, huduma ya Ndiaye pia inahitajika na Manchester United ambayo inataka kuchukua wachezaji wawili akiwemo kiungo James Garner, 25. Haijajulikana ikiwa Everton itakuwa tayari kumwachia hata mchezaji mmoja wao.