Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya kuketi kitako na Sterling

STERLING Pict

Muktasari:

  • Sterling, 31, na Axel Disasi, 27, hawajakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Stamford Bridge msimu mzima baada ya kurejea kutoka kwenye mikataba ya mkopo majira ya kiangazi yaliyopita.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Chelsea, Raheem Sterling, ambaye kwa sasa ametengwa kikosini, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya dharura na kocha mpya wa timu hiyo, Liam Rosenior, siku chache zijazo.

Sterling, 31, na Axel Disasi, 27, hawajakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Stamford Bridge msimu mzima baada ya kurejea kutoka kwenye mikataba ya mkopo majira ya kiangazi yaliyopita.

West Ham United imeulizia uwezekano wa kumsajili Sterling kwa mkopo, lakini mchezaji huyo anataka uhamisho wa kudumu, huku Fulham nao wakionesha nia.

Alipoulizwa kama tayari amezungumza na wachezaji hao wawili, Rosenior amesema: “Bado sijazungumza nao. Kumekuwa na mambo mengi sana ya kushughulikia. Nitafanya mazungumzo nao. Raheem amekuwa na taaluma ya hali ya juu sana. Nina heshima kubwa kwake, na Axel (aliyekuwa kwa mkopo Aston Villa) ni mchezaji niliyempenda kwa muda mrefu.

“Kwa idadi ya mechi tulizonazo na majukumu mengi niliyokuwa nayo, si tu upande wa mazoezi bali pia na wafanyakazi wa benchi la ufundi, bado sijafika kwenye suala hilo. Nitashughulikia hilo katika siku chache zijazo. Lazima nifanye mazungumzo nao. Lazima pia nifanye mazungumzo na klabu. Napaswa kupanga vipaumbele. Yamekuwa ni mazingira yenye msukosuko. Hilo liko karibu juu ya orodha yangu.”€Sterling alitumia msimu uliopita kucheza kwa mkopo huko Arsenal na alifunga bao moja pekee katika mechi 28.

Mchezaji mmoja ambaye Rosenior anasubiri kwa hamu kufanya naye kazi ni Cole Palmer. Amefunga mabao manne msimu huu kutokana na maumivu ya kinena. Na kwenye hilo, Rosenior amesema: “Cole ni kipaji cha kipekee. Kazi yangu ni kumfahamu, kuungana naye, na kuelewa ni nini kinachomfanya acheze kwa kiwango chake bora. Hilo linahitaji muda. Nina hamasa kubwa sana kufanya kazi naye. Kinachotisha kuhusu Cole ni kwamba tayari ana kiwango cha dunia, lakini ana umri wa miaka 23 tu. Nataka wachezaji wangu wajieleze uwanjani. Nataka wajisikie huru wakiwa ndani ya uwanja.”