Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yaendelea kumnyemelea Rashford sasa yaja na mbinu mpya

Muktasari:

  • Rashford, ambaye kwa sasa anakipiga Barcelona kwa mkopo, ameripotiwa kuivutia  PSG  kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

PARIS Saint-Germain imeanza mazungumzo na Manchester United ili kuona ikiwa kuna uwezekano wa kupata huduma ya  mshambuliaji wa timu hiyo na England, Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 28 kwa kufanya mabadilishano ya wachezaji.

Rashford, ambaye kwa sasa anakipiga Barcelona kwa mkopo, ameripotiwa kuivutia  PSG  kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mabosi wa PSG wanafahamu kwamba staa wao Bradley Barcola ni miongoni mwa mastaa ambao Man United inataka kuwasajili ili kuboresha eneo lao la kiungo, hivyo wao pia wanataka kumtumia fundi huyo kama sehemu ya ofa ya kumpata Rashford.

Hata hivyo, bado inaonekana kuna changamoto kidogo kwani Barca ina nafasi ya kumsajili staa huyu moja kwa moja kutokana ikiwa ni moja ya vipengele vilivyowekwa katika makubaliano yao na Man United wakati inamsajili staa huyu.

Mkataba wa Rashford na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu akiwa na Barca amecheza mechi 20 za michuano yote, akafunga mabao sita na kutoa asisti 10.


Sergio Reguilom

BEKI wa pembeni kutoka Hispania, Sergio Reguilon mwenye umri wa miaka 28, yuko hatua ya mwisho kukamilisha uhamisho kwenda Inter Miam kwa usajili huru baada yakukaa bila ya timu tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi alipoachwa na  Tottenham.

Inter Miami, imekuwa ikitafuta beki mwenye uzoefu wa mashindano makubwa, na Reguilón anaonekana kuwa jibu sahihi.

Ripoti zinaeleza atasaini mkataba wa miaka miwili.


Joshua Zirkzee

MANCHESTER United imekataa ombi la AS Roma la  kutaka kumsajili mshambuliaji wao Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 24, kwa mkopo nusu msimu ambao ungekuwa na kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu.

Taarifa zinaeleza kuwa Man United wako tayari kumuuza mshambuliaji huyo lakini kwa dau la moja kwa moja pekee na sio mkopo.

Mashetani hao wekundu wanataka kufanya hivyo ili fedha zitakazopatikana zisaidie katika usajili wa dirisha la Januari.


Ayyoub Bouaddi

ARSENAL imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Lille, Ayyoub Bouaddi, 18, katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.

Bouaddi ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kutoa asisti moja.


Ibrahim Konate

LIVERPOOL imeweka wazi kuwa wako tayari kupokea ofa ya takribani Pauni 15 milioni  kwa ajili ya kumuuza beki wao qa kimataifa wa Ufaransa, Ibrahima Konate mwenye umri wa miaka, 26.

Mkataba wa sasa wa Konate unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa amekataa kusaini dili jipya akionyesha dalili zote za kutaka kuondoka ifikapo mwisho wa msimu huu.

Mabosi wa Liverpool hawataki kupata hasara ya kumshuhudia akiondoka bure, hivyo inahitaji kumuuza mapema ili kupata chochote kitu.


Mohamed Salah

LICHA ya tetesi zinazoendelea mitandaoni, ripoti zinadai hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya klabu za Saudi Arabia na Liverpool kuhusu uhamisho wa  mshambuliaji Mohamed Salah, 33.

Liverpool imeendelea kusisitiza kuwa Salah bado ni sehemu muhimu ya mipango yao licha ya hivi karibuni kocha Arne Slot kumweka benchi baada ya kiwango kisichoridhisha alichoonyesha katika mechi nyingi tangu kuanza kwa msimu huu. Mkataba wa Salah unamalizika mwaka 2027.


Samu Aghehowa

TOTTENHAM Hotspur imeambiww kuwa mshambuliaji wa FC Porto, Samu Aghehowa, 21, hana nia ya kuondoka katika dirisha lijalo la Januari.

Aghehowa amekuwa miongoni mwa mastaa wanaoaminiwa sana na benchi la ufundi la Porto, na yeye mwenyewe hataki kuondoka kwa sasa akiamini bado anahitaji kumaliza msimu akiwa na  klabu hiyo kabla ya kuanza kufikiria kupata changamoto mpya sehemu nyingine.


Christos Mouzakitis

Manchester United huenda ikaangukia pua katika harakati za za kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ugiriki, Christos Mouzakitis  mwenye umri wa miaka 18, baada ya mchezaji huyo kuripotiwa kupendelea kuhamia Real Madrid badala ya timu nyingine.

Mouzakitis amekuwa akifuatiliwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya kutokana kiwango bora anachoonyesha kwa sasa akiwa na Olympiacos.

Mkataba wa sasa wa  Mouzakitis unamalizika mwaka 2029.