Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG, Barcelona jino kwa jino kwa Mason Greenwood

Muktasari:

  • Greenwood ambaye amejiunga na Marseille katika dirisha lililopita akitokea Manchester United, msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 10, akiwa na Getafe.

BARCELONA  inataka kuwasilisha ofa kwenda Marseille kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Mason Greenwood dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini wanakumbana na upinzani kutoka kwa Paris St-Germain ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Greenwood ambaye amejiunga na Marseille katika dirisha lililopita akitokea Manchester United, msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 10, akiwa na Getafe.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Greenwood amefunga mabao matano katika mechi sita za michuano yote akiwa na Marseille hali iliyozovutia timu nyingi.

Taarifa zinaeleza maskauti wa Barcelona  na PSG wamekuwa wakihudhuria mechi kadhaa za Marseille kwa ajili ya kumtazama staa huyo.

Marseille imeripotiwa kuwa tayari kumuuza staa huyu lakini kwa kiasi cha pesa kisichopungua  Pauni 60 milioni.

Mkataba wa Greenwood na Marseille unamalizika mwaka 2029.


Wakati huo huo Real Madrid ipo tayari kumuuza kiungo wao raia wa Ufaransa, Aurelien Tchouameni, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Inaelezwa Madrid ipo tayari kumuuza staa huyu kwa kiasi  kisichopungua Pauni 66 milioni ambacho timu nyingi zinaonekana kuwa na uwezo wa kuilipa. Hata hivyo, Madrid inataka kuhakikisha inamwachia ili kushusha mashine nyingine.


ASTON Villa na West Ham zinajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 25 milioni kwenda Valencia kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Mhispania Hugo Duro, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Duro ameonyesha kiwango bora tangu msimu uliopita hali iliyozivutia timu nyingi kutaka kumsajili. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na kuna uwezekano akahamia Ligi Kuu England msimu ujao.


STRAIKA wa zamani wa Manchester City na Liverpool, Mario Balotelli, 34, yupo katika mazungumzo na timu ya ligi daraja la tatu ya Hispania, CF Intercity ndani ya siku chache zijazo. Kwa sasa Balotelli yupo huru baada ya mkataba wake na Adana Demirspor ya Uturuki kuvunjika. Msimu uliopita akiwa na wababe hao wa Uturuki alicheza mechi 16 za Ligi Kuu alifunga mabao saba.


LICHA ya kupata majeraha, Manchester City bado inataka kuanza mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya kiungo wao raia wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne anayehusishwa kuwa katika rada za timu za Saudi Arabia. De Bruyne ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, amepata majeraha ambayo huenda yakamweka nje ya uwanja kwa muda.


ARSENAL inadaiwa kutaka kuipiku Liverpool kwenye dili la  kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen na timu ya Taifa ya Ujerumani,Florian Wirtz, 21, katika dirisha hili baada majogoo hao kuonekana kusua sua. Inaelezwa Liverpool imerudi nyuma kwenye dili hilo baada ya Leverkusen kuhitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza.


NEWCASTLE imefikia patamu katika mazungumzo ya mkataba mpya kati yao na wawakilishi wa Anthony Gordon unaodaiwa utamwezesha kusalia kwenye kikosi hicho hadi mwaka 2030. Hata hivyo, ripoti zinadai Newcastle inapata ugumu kwa sababu tayari timu nyingi kubwa zimeanza mazungumzo na wawakilishi wa staa huyo na zipo tayari kumpa pesa nyingi tofauti na ile ambayo wao Newcastle wanahitaji kumpa.


ARSENAL na Real Madrid zipo kwenye vita ya kuiwania saini ya beki wa kati wa  Palmeiras, Vitor Reis, 18, ambaye zinataka kumsajili katika dirisha lijalo la Januari. Reis ambaye msimu uliopita alicheza mechi 26 za michuano yote, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na kuna kila dalili akaondoka Palmeiras dirisha litakapofunguliwa na miamba hiyo imeshikana shati.