Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba afichua chanzo cha mgogoro wake na Mourinho

Muktasari:

  • Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliyerejea United 2016 kwa ada ya rekodi ya Euro 89 milioni akitokea Juventus aliingia kwenye migogoro kadhaa ya wazi na Mourinho kabla ya kocha huyo kufutwa kazi Desemba 2018.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa boli, Paul Pogba anaamini kuwa maswali ya mara kwa mara kutoka kwa vyombo vya habari kuhusu majeraha yake na mustakabali wake katika kikosi cha Manchester United yalichangia kumkera kocha Jose Mourinho na kusababisha kuvunjika kwa uhusiano wao Old Trafford.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliyerejea United 2016 kwa ada ya rekodi ya Euro 89 milioni akitokea Juventus aliingia kwenye migogoro kadhaa ya wazi na Mourinho kabla ya kocha huyo kufutwa kazi Desemba 2018.

Akizungumza kwenye podikasti ya beki wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand, Pogba ambaye kwa sasa yupo AS Monaco baada ya kurejea uwanjani kufuatia kufungiwa miezi 18 kwa kosa la kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, alisema matatizo yao yalianza kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamuandama mara kwa mara jambo ambalo Mourinho hakulifurahia.

“Tulikuwa na uhusiano mzuri mwanzoni tukitumiana ujumbe na mambo kama hayo. Yeye ni mtu wa kuchekesha sana, lakini baada ya muda, majeraha yalibadilisha mambo. Vyombo vya habari vilikuwa vinamuuliza sana kuhusu mimi ‘Paul, Paul, Paul’ na hilo linawezekana lilimkera,” ,” alisema Pogba.

Nyota huyo pia aliwahi kudai kuwa uhusiano huo ulianza kudorora zaidi baada ya Mourinho kutuma picha yake kwa wakala wake, hayati Mino Raiola, wakati alipokuwa akijiuguza majeraha na ilidaiwa kocha huyo alitilia shaka safari yake ya kujiuguza nchini Marekani na hata kutuma picha akiwa na mkewe Zulay huko Miami.

Baadaye, Mourinho alimvua Pogba unahodha msaidizi na kutoa kauli zisizo za moja kwa moja kuhusu kiwango chake akiwa timu ya taifa, kabla ya mzozo wao mazoezini kunaswa na kamera. Pia inadaiwa alimuita Pogba “kirusi”, kauli ambayo haikupokewa vizuri na mchezaji huyo.

“Kila kitu kilibadilika,” alisema Pogba, ambapo pia alizungumzia tofauti kubwa kati ya kipindi chake cha kwanza United na kurejea kwake baadaye, ambapo alikaririwa na rafiki yake Patrice Evra kuwa mazingira ya klabu yalikuwa yamebadilika.

“Nilimwambia Pat kila kitu ni tofauti. Nguvu, mazingira hata chakula. Haikuwa ileile. Nilihisi kama siyo klabu ile niliyoiacha,” alisema Pogba na kuongeza kuwa mapema baada ya kurejea alikuwa na shaka kama angemaliza mkataba wake.

Pogba alimaliza mkataba wake United kabla ya kuondoka bure 2022 kurejea Juventus. Hata hivyo, kipindi chake Italia kilikumbwa na majeraha na adhabu ya dawa za kusisimua misuli, kabla ya kurejea tena uwanjani na kujiunga na Monaco kwa mkataba wa miaka miwili.