Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pochettino atajwa kurudi Tottenham Hotspur

SPURS Pict

Muktasari:

  • Pochettino mwenye umri wa miaka 53 kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Marekani, moja ya waandaji wa Kombe la Dunia 2026 na inadaiwa amegoma kuachana na mradi huo ili kwenda kuifundisha Tottenham.

LONDON, ENGLAND: MABOSI wa Tottenham Hotspur wanadaiwa kuwa katika mpango wa kutaka kumrejesha Mauricio Pochettino katika msimu ujao baada ya kumfuta kazi kocha Thomas Frank.

Pochettino mwenye umri wa miaka 53 kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Marekani, moja ya waandaji wa Kombe la Dunia 2026 na inadaiwa amegoma kuachana na mradi huo ili kwenda kuifundisha Tottenham.

Spurs ilimfukuza Frank, raia wa Denmark mwenye miaka 52, wiki hii baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwa kipindi cha miezi minane.

Klabu hiyo ya Kaskazini mwa London iko nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu  England ikiwa na tofauti ya pointi tano dhidi ya timu tatu za mwisho.

Frank aliiongoza Spurs kupata ushindi katika mechi mbili tu kati ya 17 za mwisho za ligi na mechi yake ya mwisho ilikuwa ni kipigo cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Newcastle United, Jumanne.

Pochettino, aliyewahi kuinoa Spurs na kuifikisha klabu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 na kuwafanya wapambane kileleni mwa Ligi Kuu kwa kipindi cha miaka mitano kati ya 2014–2019, anaelezwa kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa timu hiyo wanaotamani arudi.

Jina la kocha huyo raia wa Argentina liliimbwa na mashabiki Jumanne wakati Spurs ikiendelea kuzama kutokana na kipigo kutoka Newcastle.

Hata hivyo, inaonekana kuwa ni ngumu kwa sababu anaiandaa Marekani kuelekea Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Inaaminika kuwa kocha huyo wa zamani wa Chelsea yuko tayari  kurejea Spurs mara tu mkataba wake na timu ya taifa ya Marekani utakapomalizika katika majira ya kiangazi mwaka huu.

Kocha wa zamani wa Brighton, Roberto De Zerbi, aliyeachana na Marseille juzi naye anapigiwa upatu kuchukua kibarua hicho pamoja na makocha wengine wakubwa kama, Marco Silva na Xavi Hernandez.

Tottenham ina mapumziko ya siku kumi kabla ya mchezo wao wa dabi ya Kaskazini mwa London nyumbani dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Arsenal.