Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs haijawahi kutokea

SPURS Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Spurs anashikilia rekodi ya kuwa na wastani mdogo zaidi wa pointi kwa mchezo (PPG) na asilimia ndogo zaidi ya ushindi kati ya makocha wote wa Big Six waliocheza michezo 10 au zaidi ya Ligi Kuu.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Tottenham, Thomas Frank ndiye kocha mwenye rekodi mbaya zaidi katika historia ya Ligi Kuu England kwa zile timu sita kubwa.

Kocha huyo wa Spurs anashikilia rekodi ya kuwa na wastani mdogo zaidi wa pointi kwa mchezo (PPG) na asilimia ndogo zaidi ya ushindi kati ya makocha wote wa Big Six waliocheza michezo 10 au zaidi ya Ligi Kuu.

Hesabu hiyo inawaondoa makocha wa mpito (interim/caretaker), pamoja na makocha wa Manchester City kabla ya timu haijanunuliwa na matajiri wa Abu Dhabi na wale wa Tottenham kabla ya ujio wa Harry Redknapp.

Kwa kuangalia vipindi vya makocha katika Ligi Kuu kwa Chelsea, Arsenal, Manchester United, Manchester City, Tottenham na Liverpool, Frank yuko mkiani kabisa.

Katika mechi 25 alizoiongoza Spurs msimu huu, Frank amekusanya pointi 29 tu. Hilo linaiacha timu yake ikiwa imeshika nusu ya chini ya msimamo wa ligi, huku West Ham walioko nafasi ya 18 (eneo la kushuka daraja) wakiwa pointi sita tu nyuma yao.

Spurs wako katika hatari ya kuingia katika vita ya kuepuka kushuka daraja pamoja na Leeds, Nottingham Forest na Crystal Palace.

Baada ya kupoteza dhidi ya Man United, Frank alikuwa amefikisha mechi saba mfululizo bila ya kupata ushindi, pia aliweka rekodi ya kushinda mechi mbili tu kati ya 16.

Baada ya Ange Postecoglou kumaliza msimu uliopita vibaya, Frank kwa ujumla anaendelea kufanya vibaya zaidi kuliko mtangulizi wake.

Postecoglou alishinda Europa League katika msimu wake wa pili, akiiwezesha Spurs kufuzu Ligi ya Mabingwa kupitia njia hiyo baada ya kushindwa kumaliza nafasi nne za juu.

Postecoglou yuko nafasi ya tano katika orodha hii akiwa na wastani wa pointi 1.37 kwa mchezo (PPG) katika mechi 76, akishinda asilimia 40 ya michezo hiyo.

Frank ana asilimia 28 ya ushindi, ambayo pia ni ya chini zaidi, chini hata ya Ruben Amorim alipokuwa Manchester United.

Amorim alifutwa kazi si kwa sababu ya matokeo pekee bali pia mvutano wake na Jason Wilcox, lakini bado alipata asilimia 23 tu ya ushindi na wastani wa pointi 1.23 kwa mchezo.

Kocha wa zamani wa Liveprool, Roy Hodgson ambapo ligi ilikuwa ikichezwa mechi 20  anashika nafasi ya tatu kwa kufanya vibaya, akiwa na wastani wa pointi 1.25 kwa mchezo na asilimia 35 ya ushindi.

Graham Potter akiwa Chelsea aliyoiongoza kwa mechi 22, alikuwa bora kidogo kwa wastani wa pointi 1.27 alikuwa na asilimia mbaya za ushindi (21).