Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yamfuta kazi kocha wake Frank

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 52 alichukua mikoba ya kuonoa Spurs kutoka kwa Ange Postecoglou wakati wa majira ya kiangazi ya mwaka jana.

LONDON, ENGLAND: KOCHA, Thomas Frank amefutwa kazi ya kuinoa Tottenham Hotpur kutokana na kikosi hicho kupata matokeo ya hovyo.

Kocha huyo raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 52 alichukua mikoba ya kuonoa Spurs kutoka kwa Ange Postecoglou wakati wa majira ya kiangazi ya mwaka jana.

Lakini, katikati ya msimu wake wa kwanza akiwa kocha mkuu kwenye Uwanja wa N17, ameondolewa katika wadhifa wake.

Frank alishindwa kuwashawishi mashabiki wa Spurs na alipata vipigo muhimu nyumbani dhidi ya Bournemouth, Aston Villa, Fulham na West Ham. Ushindi huo wa West Ham uliopatikana kupitia bao la Callum Wilson katika dakika za majeruhi ulikuwa wa kwanza kwao katika mechi 11.

Na hali hiyo iliongeza presha kwa bodi ya Tottenham kumfuta kazi Frank.

Matokeo hayo ya kushtua yalikuwa ni kipigo cha tatu mfululizo ikiwa ni pamoja na kutolewa kwenye Kombe la FA na yaliiacha Spurs ikiwa na ushindi mmoja tu katika mechi nane. Mambo yaliendelea kuwa mabaya tangu mechi hiyo. Kulikuwa na mwanga wa matumaini kwamba Spurs ingeweza kugeuza msimu wao baada ya ushindi wa kushawishi wa 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na ushindi wao dhidi ya Frankfurt wiki iliyofuata katika mashindano hayo.

Lakini, sare ya kukatisha tamaa ya 2-2 dhidi ya Burnley, sare dhidi ya wanaowania ubingwa Manchester City na kipigo kutoka kwa Manchester United vilirejesha presha kwa Frank kabla ya kuchapwa tena usiku wa Jumanne baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Newcastle.

Mambo nje ya uwanja nayo hayakumsaidia kocha huyo, huku nahodha Cristian Romero akiishambulia klabu kwa kile alichokiita aibu ya kutosajili wachezaji dirisha la usajili wa majira ya baridi lilipofungwa. Romero aliongeza matatizo ya Frank alipotolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Man United na kulazimika kutumikia adhabu ya mechi nne, hali iliyoiacha timu bila huduma ya mmoja wa wachezaji wao bora msimu huu.