Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji Liverpool anajua tatizo la Wirtz

WITZ Pict

Muktasari:

  • Liverpool imelipa Pauni 100 milioni za awali na italazimika kulipa Pauni 16 milioni nyingine za ziada baada ya kunasa saini ya kiungo Wirtz kutoka kwenye kikosi cha Bayer Leverkusen katika dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

LIVERPOOL, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Ligi Kuu England, Danny Murphy amefunguka anafahamu ni kitu gani kinachomfanya Florian Wirtz wa Liverpool ashindwe kufanya vizuri tangu aliponaswa kwa pesa nyingi kutokea Ujerumani.

Liverpool imelipa Pauni 100 milioni za awali na italazimika kulipa Pauni 16 milioni nyingine za ziada baada ya kunasa saini ya kiungo Wirtz kutoka kwenye kikosi cha Bayer Leverkusen katika dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Licha ya kuasisti bao la Hugo Ekitike kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Crystal Palace zaidi ya miezi miwili iliyopita, Wirtz ameshindwa kufunga wala kuasisti tangu wakati huo.

WIT 02

Kiwango chake akicheza Namba 10 na winga kimezua mjadala mkubwa kutoka kwa wachambuzi.

Lakini, staa wa zamani wa Liverpool, Murphy amesema: “Tukimzungumzia Wirtz, wiki moja anacheza na Ekitike na wiki nyingine anacheza na Isak.  Amekuwa pia akichanganyiwa pacha wa kucheza nao kwenye sehemu ya kiungo wakati yeye akicheza kama Namba 10, mpira unaanza kujenga ushirikiano na viungo. Nani atanipa mpira haraka, nani naweza kumwaamini na kumpa mpira. Hapo ndipo unapozungumzia mfano wa Wirtz.

WIT 01

“Nadhani ishu nyingine pia ni kuendana na kasi ya Ligi Kuu England. Anahitaji kuwa tayari kiakili na kimwili.”