Perez ampotezea Ronaldo

MADRID, HISPANIA. RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amempotezea, Cristiano Ronaldo akidai hana hana mpango wa kumsajili kwani umri wake umekwenda.
Kauli hiyo aliisema baada ya mashabiki kumuuliza endapo klabu hiyo ina mkakati wa kumrejesha Ronaldo mwenye umri wa miaka 38.
Nyota huyo anayekipiga Manchester United aliigomea klabu hiyo anataka kuondoka dirisha hili la usajili, hata hivyo mabosi wamegoma kumuuza.
Aidha kwa upande wa Perez alipuuzia wazo la mashabiki kuhusu uwezekano wa Ronaldo kurudi Los Blancos lakini akajibu “
“Kumsajili Cristiano, tena?, hapana kwasasa ana umri wa miaka 38,”
Mpaka sasa miamba hiyo ya Hispania imemsajili kiungo Aurelien Tchouameni kutoka Monaco kwa kitita cha Pauni 85 milioni, pamoja na Antonio Rudiger akitokea Chelsea kwa uhamisho huru.