Pep Guardiola, Semenyo lolote linatokea
Muktasari:
- Manchester City inapewa nafasi kubwa ya kumsajili winga huyo wa Bournemouth, ambaye kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachotaja bei anayouzwa ni Pauni 65 milioni.
MANCHESTER, ENGLAND: PEP Guardiola atakuwa bize dirisha la Januari huku staa Antoine Semenyo akiripotiwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji inayopanga kuwasajili katika uhamisho huo wa majira ya baridi huko Ulaya.
Manchester City inapewa nafasi kubwa ya kumsajili winga huyo wa Bournemouth, ambaye kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachotaja bei anayouzwa ni Pauni 65 milioni.
Pep mara zote amekuwa mgumu kutumia pesa dirisha la Januari, lakini alitumia Pauni 174.2 milioni iliposajili wachezaji watano mwanzoni mwa mwaka huu.
Ikielekea Januari 2026, Man City ipo kwenye msako wa mataji manne, hivyo Guardiola anaweza kufungua pochi kunasa mastaa wa kuja kuboresha kikosi chake.
Guardiola amesema: “Msimu uliopita, sikuwa na matarajio ya kwenda kwenye dirisha la uhamisho na kusajili wachezaji wanne au watano. Lakini, tulipata majeruhi wengi sana. Mwaka huu chochote kinaweza kutokea.”
Man City itakabiliwa na vita kali kutoka kwa Liverpool katika msako wa kumsajili supastaa huyo wa kimataifa wa Ghana, ambaye atatimiza umri wa miaka 26, Januari 7.
Guardiola anafahamu wazi atahitaji kuboresha kikosi chake kama Man City inahitaji kufanya kweli kwenye ligi na mashindano mengine inayoshiriki miamba hiyo ya Etihad