Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe kiboko ya Bale ni Richards

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Tottenham Hotspur na Wales, Bale amekuwa na kipindi kizuri kwenye soka, akishinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tano, La Liga mara tatu kwa kipindi chake alichokuwa akikipiga Real Madrid.

LONDON, ENGLAND: GARETH Bale amefunguka Micah Richards ndiye beki mgumu zaidi aliyekuwa akimpa shida uwanjani wakati walipokuwa wakikipiga.

Gwiji huyo wa Tottenham Hotspur na Wales, Bale amekuwa na kipindi kizuri kwenye soka, akishinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tano, La Liga mara tatu kwa kipindi chake alichokuwa akikipiga Real Madrid.

Alistaafu soka Januari 2023, baada ya kushinda Kombe la MLS alipokuwa na Los Angeles FC. Wakati anajibu maswali ya papohapo, Bale aliulizwa ni beki gani alikuwa anampa wakati mgumu uwanjani, staa huyo hakung'ata vidole, alijibu: “Micah Richards.”

Beki huyo wa kulia wa zamani wa Manchester City, Richards nyakati zake za uwanjani zilikatishwa mapema kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti na hivyo kustaafu mwaka 2019, wakati akiwa na umri wa miaka 31.

Lakini, hadi kipindi hicho Richards anastaafu soka, tayari alikuwa ameshabeba taji la Ligi Kuu England mara mbili, Kombe la FA na Kombe la Ligi. Alishuka daraja pia na kwenda kucheza kwenye Championship alipokuwa Aston Villa na alikwenda kucheza kwa mkopo kwa msimu mzima huko Italia katika kikosi cha Fiorentina cha Serie A.

Richards tangu wakati huo sasa amegeukia kwenye kazi ya uchambuzi wa mechi za soka. Bale, 36, alikutana na Richardd mara tano ndani ya uwanja, lakini alishinda mara moja tu, huku kikosi chake kilikumbana na kipigo kwenye mechi tatu.

Bale alisema pia bao lake bora zaidi alilowahi kufunga ni lile la ticktack kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool mwaka 2018, wakati alipokuwa akicheza Real Madrid.

Staa Bale alisema mchezaji mwenzake mwenye kipaji zaidi aliyewahi kucheza naye ni Cristiano Ronaldo, huku kocha bora ni Pep Guardiola, wakati bao bora kwenye Ligi Kuu England ni lile lililofungwa na gwiji wa Arsenal, Dennis Bergkamp dhidi ya Newcastle United.