Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep akumbushia mkataba wake Man City

PEP Pict

Muktasari:

  • Man City pia wanatajwa kuwa tayari wameanza kujipanga na kuondoka kwake na kocha wa zamani wa Chelsea ,Enzo Maresca anatajwa kuwa mmoja wa makocha wanaoweza kuchukua nafasi yake.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ametuma ujumbe mzito kwa wanaodhani anaweza kuondoka klabuni hapo hivi karibuni baada ya kukumbusha bado ana mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wake wa sasa.

Mustakabali wa Guardiola umekuwa gumzo kubwa katika wiki za karibuni, huku taarifa zikidai huenda akabwaga manyanga mwisho wa msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 10 yenye mafanikio makubwa.

Man City pia wanatajwa kuwa tayari wameanza kujipanga na kuondoka kwake na kocha wa zamani wa Chelsea ,Enzo Maresca anatajwa kuwa mmoja wa makocha wanaoweza kuchukua nafasi yake.

Guardiola aliiongoza Man City kucheza fainali ya FA wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea na kuchukua taji hilo baada ya ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Antoine Semenyo dakika 71.

PE 02

Hilo lilikuwa ni taji la 20 kwa Guardiola ambaye kwa msimu huu tayari ameshachukua mawili akianzia na lile la Carabao Cup alilochukua mbele ya Arsenal.

Kwa sasa macho na masikio yapo Ligi Kuu England ambako wanakimbizana na washika mitutu wa Jiji la London, Arsenal ambao ndio vinara kwa sasa.

Mapema mwezi huu Guardiola amesema bado ana nguvu kubwa sana ya kuendelea kuinoa Manchester City licha ya tetesi zinazodai ataondoka.

“Nisingekaa miaka 10 hapa na kupata mafanikio yote haya yote kama ningechoka mapema. Bado nina nguvu kubwa sana, bado ninajisikia vizuri sana, hata siku zangu za mapumziko ninakuja kufanya kazi,” amesema Guardiola.

PE 01

“Ni kweli tupo hapa kwa sababu tumeshinda mataji mengi na ndiyo maana hawakunifukuza kazi kwa sababu wanaendelea kuniamini. Lakini zaidi ya hilo, klabu hii ni ya kipekee sana. Watu hapa wanatutunza kwa kila kitu hata mambo madogo madogo.

"Mambo madogo ndiyo yanayofanya kazi yangu kama kocha na ya wachezaji iwe rahisi kwa sababu tunabaki kufikiria tu kuhusu kazi yetu. Ni kama mazingira ya familia yanayowafanya watu wajisikie vizuri.

"Ni klabu kubwa lakini hapa ni kama familia. Wachezaji wanaweza kuvunjika moyo kwa kutocheza, hilo ni jambo la kawaida na linaeleweka. Lakini zaidi ya hapo, hakuna mtu anayeweza kulalamika."