Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pauni 1.56 bilioni zaipaisha Chelsea, yatajwa kuwa kinara

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Wachambuzi kutoka chuo cha masuala ya michezo cha CIES Football Observatory kilichopo, Switzerland wametoa ripoti inayoonyesha  kuwa kikosi cha Enzo Maresca chenye maskani yake Stamford Bridge kinathamani Pauni 1.56 bilioni.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya usajili wa maana uliofanywa kwa takribani misimu miwili,  Chelsea imekuwa timu yenye thamani kubwa zaidi duniani katika soka.

Wachambuzi kutoka chuo cha masuala ya michezo cha CIES Football Observatory kilichopo, Switzerland wametoa ripoti inayoonyesha  kuwa kikosi cha Enzo Maresca chenye maskani yake Stamford Bridge kinathamani Pauni 1.56 bilioni.

Hii ni takriban Pauni 100 milioni zaidi ya kikosi cha Real Madrid kilichopo nafasi ya pili katika orodha hiyo ya vikosi vyenye thamani zaidi duniani ambayo inaonyesha klabu saba za Ligi Kuu England zikiwa kwenye nafasi 12 za juu.

Tangu uongozi wa Boehly na matajiri wenzake uchukue umiliki wa Chelsea mwaka 2022, baada ya Roman Abramovich kulazimishwa kuuza hisa zake, klabu hiyo imetoa takribani  Pauni 1.5 bilioni kama ada za kununua wachezaji.

CHEL 01

Pesa hizo pia ni mjumuisho wa ada zilizitolewa katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi kununua mastaa kibao ikiwemo Joao Pedro, Estevao Willian, Alejandro Garnacho, Liam Delap na Jamie Gittens.

Licha ya kwamba thamani ya kikosi, imejumuisha pia na pesa zilizopatikana kwa kuuza wachezaji wengine, kwa dirisha lililopita pekee tu, Chelsea ilitumia takribani Pauni 315 milioni kununua wachezaji wapya na kulipa mawakala.

Nguvu ya kifedha ya timu za Ligi Kuu England pia imeonekana katika orodha hiyo ambapo klabu zote 20 za ligi hiyo zipo katika nafasi 60 za juu kwa kuwa na vikosi vyenye thamani zaidi duniani.

Manchester City ipo nafasi ya tatu kwenye orodha hiyo ikiwa na thamani ya Pauni 1.28 bilioni, ikifuatiwa kwa karibu na Arsenal, yenye thamani ya Pauni 1.27 bilioni katika nafasi ya nne.

Liverpool, ipo  nafasi ya sita kwa kikosi chenye thamani ya Pauni  1.21 bilioni, baada yake ni Tottenham, iliyoko nafasi ya nane na Man United ipo nafasi ya 12 ikiwa na wachezaji wenye thamani ya Pauni 710 milioni.