Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Partey arudi London kujibu kesi mpya ya ubakaji

PARTEY Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal amekana mashtaka mawili mapya ya ubakaji katika Mahakama ya Southwark Crown ambayo yalifunguliwa miezi michache iliyopita.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey, amerudi mahakamani jijini London, na amekana mashtaka mapya mawili ya ubakaji yanayomhusu mlalamikaji mpya.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal amekana mashtaka mawili mapya ya ubakaji katika Mahakama ya Southwark Crown ambayo yalifunguliwa miezi michache iliyopita.

Partey mwenye umri wa miaka 32 anatuhumiwa  kuwabaka wanawake wawili na kumshambulia kingono mwingine wa tatu.

Mwezi Februari alishtakiwa kwa mashtaka mawili ya ziada ya kumbaka mwanamke mwingine  Desemba 2020, na alifika mahakamani mchana leo kujibu mashtaka hayo.

Akizungumza kuhusu mashtaka hayo mapya wakili wa utetezi, Jenny Wiltshire, amesema: “Thomas Partey anaendelea kukana mashtaka yote dhidi yake. Amekuwa akishirikiana na polisi wakati wote. Kutokana na kuwa kuna kesi inaendelea mahakamani hakutakuwa na maoni zaidi.”

Partey alishtakiwa mwaka jana kwa makosa matano ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili na kosa la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mlalamikaji wa tatu, kufuatia uchunguzi wa Polisi wa Metropolitan.

Tayari amekana mashtaka yote hayo yanayohusu matukio ya mwaka 2021 na 2022, na anatarajiwa kusikilizwa kesi katika Mahakama ya Southwark Crown mwezi Novemba.

Mwezi Februari, mashtaka mawili mapya ya ubakaji yalijitokeza .

Katika mashtaka hayo mapya, kiungo huyo wa Ghana ambaye kwa sasa anachezea Klabu ya Villarreal ya Hispania anadaiwa kumbaka mwanamke mara mbili jijini London siku moja ya Desemba 2020.

Mwendesha mashtaka, Arabella MacDonald, aliiambia mahakama mwezi Februari: “Bw. Partey anakabiliwa na mashtaka mawili ya ziada ya ubakaji yanayohusiana na Desemba 2020.

Mlalamikaji alijitokeza baada ya taarifa za kesi nyingine kusambaa kwa umma.”

Mwanasoka huyo ambaye awali alikuwa akiishi Potters Bar, Hertfordshire, alijiunga na Arsenal kutoka Atletico Madrid 2020 kwa ada ya uhamisho ya takriban Pauni 45 milioni kabla ya kuondoka klabuni hapo Juni, mwaka jana, baada ya mkataba wake kumalizika. Alicheza mechi 167 katika misimu mitano akiwa Arsenal.