Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Partey akabiliwa na mashtaka mapya mawili ya ubakaji

Muktasari:

  • Kesi ya nyota huyo ilisikilizwa juzi, huku mwenyewe akiwa hayupo mahakamani. Kwa sasa anaitumikia Villareal ya Hispania.

LONDON, ENGLAND: Thomas Partey, mchezaji wa zamani wa Arsenal, anatarajiwa kupinga mashtaka mawili mapya ya ubakaji yaliyowasilishwa dhidi yake, mahakama imeelezwa.

Kesi ya nyota huyo ilisikilizwa juzi, huku mwenyewe akiwa hayupo mahakamani. Kwa sasa anaitumikia Villareal ya Hispania.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 alishtakiwa mwezi uliopita kwa makosa mawili ya ubakaji anayodaiwa kuyafanya kwa mwanamke mmoja wakati wa miadi Desemba 2020.

Katika Mahakama ya Hakimu ya Westminster, Partey hakuhudhuria wakati Naibu Hakimu Mkuu, Tan Ikram alipokuwa akishughulikia hatua za awali za kesi hiyo.

Mwanasoka huyo aliruhusiwa kutohudhuria, lakini wakili wake, Emma Fenn, aliashiria kuwa mteja wake atakana mashtaka yote mawili. Mashtaka mengine yaliyotangulia ni yale ya mwaka uliopita ambapo Partey pia alishtakiwa kwa makosa matano ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili na kosa moja la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke wa tatu, kufuatia uchunguzi wa Polisi wa Metropolitan.

Tayari amewasilisha maelezo ya kutokiri mashtaka yanayodaiwa kutokea kati ya 2021 na 2022. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kuanza kesi kamili huko Southwark Crown, mwezi Novemba, mwaka huu.

Mahakama ilielezwa kuwa mashtaka mapya mawili ya ubakaji yalijitokeza baada ya yale ya awali kuwekwa hadharani.

Mwendesha mashtaka, Arabella MacDonald alisema: “Partey anakabiliwa na mashtaka mawili zaidi ya ubakaji yanayodaiwa kutokea Desemba 2020. Mlalamikaji alijitokeza baada ya habari za kesi nyingine za Partey kusambaa sana kwenye vyombo vya habari.”

Hakimu Ikram aliamuru mashtaka hayo mapya yapelekwe katika mahakama ya juu kwa usikilizwaji Aprili 10.

Katika mashtaka hayo mapya, kiungo huyo wa Ghana anatuhumiwa kumbaka mwanamke mara mbili mjini London.

Partey aliwahi kuishi Potters Bar na alijiunga na Arsenal 2020 akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia Pauni 45 milioni. Masharti ya dhamana ni kwamba Partey hatakiwi kuwasiliana na mlalamikaji. Anatarajiwa kuhudhuria usikilizwaji unaofuata wa kesi mwezi Aprili.