Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Partey apewa kesi mpya ya kubaka

PARTEY Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa anakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kukana kuwabaka wanawake wawili na kumshambulia kingono mwanamke wa tatu.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey, amefunguliwa mashtaka mengine ya ubakaji.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa anakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kukana kuwabaka wanawake wawili na kumshambulia kingono mwanamke wa tatu.

Sasa Partey ameshtakiwa kwa makosa mawili zaidi ya ubakaji yanayohusiana na mwanamke mwingine wa ziada.

Ofisi ya Mashtaka ya Umma imesema mashtaka hayo mapya yameletwa kufuatia uchunguzi mpya wa Polisi wa Metropolitan.

Msemaji amesema tuhuma hizo ziliripotiwa kwa mara ya kwanza Agosti 2025. Partey atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Westminster, Machi 13 mwaka huu. Kiungo huyo alikana mashitaka matano ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono, Septemba mwaka jana. Inadaiwa alitenda makosa hayo kati ya mwaka 2021 na 2022.

Nyota huyo, anayetarajiwa kusafiri na Ghana kwenda Kombe la Dunia 2026 wakati wa majira ya kiangazi, anatarajiwa kusimama kizimbani Novemba 2 mwaka huu. Mkataba wa Partey na Arsenal ulimalizika, Juni 30 mwaka jana na haukuongezwa jambo lililomfanya kuwa mchezaji huru. Tangu wakati huo alijiunga na klabu ya La Liga ya Villarreal.

Wakili wa utetezi wa Partey, Jenny Wiltshire, amesema: “Thomas Partey anaendelea kukana mashtaka yote dhidi yake. Ameshirikiana kikamilifu na polisi katika kipindi chote cha uchunguzi. Kwa kuwa kuna mchakato wa kisheria unaoendelea, hakutakuwa na maoni zaidi.”

Uchunguzi dhidi ya kiungo huyo wa ulinzi ulianza Februari 2022 baada ya polisi kupokea taarifa ya kwanza ya ubakaji.

Ofisi ya Mashtaka ya Umma ilisema mashtaka hayo yameletwa baada ya “kupitia kwa makini jalada pana la ushahidi.”

Partey alikuwa katika klabu ya Arsenal kwa miaka mitano baada ya kusaini mwaka 2020 akitokea Atletico Madrid, ambapo alishinda taji la Europa League.