Palmer bado kizunguzungu Chelsea FC
Muktasari:
- Staa wa The Blues, Palmer, 23, ametumika kwenye mechi nne tu za michuano yote msimu huu. Palmer alipata maumivu hayo katika kipindi cha pre-season cha Chelsea.
LONDON, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Chelsea itaendelea kuikosa huduma ya kiungo wake fundi wa ushambuliaji, Cole Palmer hadi mwezi Novemba kutokana na kusumbuliwa maumivu ya misuli ya kinena.
Staa wa The Blues, Palmer, 23, ametumika kwenye mechi nne tu za michuano yote msimu huu. Palmer alipata maumivu hayo katika kipindi cha pre-season cha Chelsea.
Palmer alicheza kwa dakika zote 90 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England msimu huu wakati kikosi hicho cha Enzo Maresca kilipotoka sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace.
Lakini, tatizo hilo la maumivu ya misuli limemfanya akose mechi dhidi ya West Ham na Fulham, katika kuelekea mapumziko ya mechi za kimataifa za Septemba.
Palmer alirejea benchini kwenye mechi dhidi ya Brentford, Septemba 13, alipoonyesha kiwango bora na kufunga kwenye sare ya 2-2. Alifunga tena bao kwenye kipigo cha 3-1 dhidi ya Bayern Munich siku nne baadaye, ambapo alicheza kwa dakika 90.
Jumamosi iliyofuatia, Palmer alitolewa uwanjani katika dk21 ya mechi ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester United, ambapo kocha Maresca alikuwa tayari alishafanya mabadiliko ya Pedro Neto na Estevao Willian baada ya kipa Robert Sanchez kuonyeshwa kadi nyekundu.
Maumivu hayo ya kinena yamemfanya Palmer kuwa nje ya kambi ya timu ya taifa ya England mara zote mbili msimu huu.
Kocha wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel alibainisha kwamba wasiwasi wake juu ya maumivu hayo ya Palmer yanaweza kuwa sugu. Lakini, taarifa za kutoka huko Stamford Bridge, Chelsea inaamini staa huyo atarudi uwanjani Novemba.
Madaktari wa Chelsea hawatarajii kumfanyia upasuaji Palmer ili kumaliza tatizo hilo ikiamini kwamba atapona maumivu yake bila ya shida.
Chelsea inatarajia kumkosa staa huyo kwenye mechi zao dhidi ya Nottingham Forest, Ajax, Sunderland na Wolves.ani huo.